ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 18, 2017

MBAO WAMILIKI BASI LAO.


Klabu ya Mbao FC imeingia kwenye orodha ya klabu zinazomiliki usafiri wake.
Mapema leo Mbao Fc leo imekabidhiwa basi na wadhamini wake kampuni ya GF Trucks & Equipment LTD.


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angella Mabula ambaye amekuwa akiunga mkono michezo katika mkoa wa Mwanza alikuwepo kukabidhiwa.


Heshima kwa klabu hiyo imekuja nao wadhamini kuanza kuiamini kutokana na mafanikio ya muda mfupi waliyoweza kuyavuna huku wakishikilia imani ya kutandaza soka zaidi na kujiepusha na  migongano ya ndani huku klabu hiyo ikiweka mfumo mzuri wa kiuongazi na usajili wa wachezaji.
Mbao Fc sasa imekuwa ni moja kati ya vilabu vinavyo aminika kama kiboko ya vigogo kutokana na kuvihenyesha vilabu vikubwa na kuzipa wakati mgumu timu nyingine shiriki za Ligi kuu Soka  Vodacom Tanzania Bara.
 Na tusherehekeee...............!!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.