Kutokea mkoani Kigoma leo July 21, 2017 amefanya ziara yake ya kikazi
ikiwa ni pamoja na kuzindua mradi wa barabara ya Nyakanazi – Kibondo
pamoja na Kidahwe – Kasulu, Rais Magufuli amezungumza mambo mengi kwenye
hotuba yake ikiwemo kodi, barabara, alivyojitoa kwa Tanzania na
mengine.
"Tumeibiwa sana madini, tumewaita waje tuzungumze wakichelewachelewa nitafunga migodi yote, mara kumi wapewe Watanzania" - JPM
'Kuanzia tarehe 1 mwezi wa 7, 2017 ukibeba mazao hautatozwa ushuru sio kwa gunia tu, hata tani 1 ya gari'' -Rais Magufuli
'Nataka ifike wakati mtu atoke hapa Nyakanazi hadi Dar es Salaam kwa bajaji kwenye lami na hili linawezekana kabisa' - Rais Magufuli
'Nilipokea malalamiko ujenzi unakwenda taratibu mkandarasi asinijaribu, mimi kufukuza makandarasi ni kama kunywa chai'' - Rais Magufuli
''Niwambie ukweli, fedha nyingi zinapotelea serikalini, ndiomana
nimezuia semina, posho za ajabu, safari hadi nikupe kibali'' - Rais
Magufuli
''Tulipoingia tulikuwa tunakusanya kodi bilioni 800 tukabana tukapata trilioni 1.3, tukibana zaidi tutapata hadi trilioni 3'' -Rais Magufuli
''Tumeondoa tozo katika sekta za mifugo, uvuvi na kilimo ili kutimiza ahadi ya kuwatumikia wananchi'' - Rais Magufuli
''Na nyinyi wananchi msinyamaze, toeni ushirikiano kuondoa tatizo la ujambazi'' - Rais Magufuli
''Mkandarasi fanya kazi usiku na mchana barabara hii ya Kibondo - Nyakanazi ikamilike kwa haraka'' - Rais Magufuli
''Waziri wa Fedha hakikisha mkandarasi analipwa haraka ili tumalize mradi huu haraka iwezekanavyo' -Rais Magufuli
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.