Naibu Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla
akitoa maelekezo kuhakikisha boma hilo la chumba cha upasuaji linakamilika
ndani ya miezi minne.
Dk.
Kigwangalla apiga tafu ujenzi wa jengo la Makao makuu ya CCM Mkoa wa Songwe
Na Mwandishi
Wetu, Songwe
Mbunge wa
Nzega Vijijini ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashahuri Kuu ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) Taifa, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, ametembelea kujionea maendeleo ya ujenzi wa
Boma la jengo la ofisi za chama hicho kwa Mkoa wa Songwe huku akichangia kiasi
cha shilingi Laki Tano.
Dk.
Kigwangalla ambaye yupo kwenye ziara ya kikazi kwenye Mkoa huo mpya kwa ajili
ya kukagua huduma za Afya ambapo alipata wasaha huo wa kutembelea jengo hilo na
kueleza kuwa Serikali ya awamu ya tano ya CCM,
itaendelea kuboresha huduma bora
za afya kama Ilani inavyosema ambapo aliwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli katika juhudi zake
mbalimbali za kulinda rasilimali za nchi.
“Rais wetu
ameongeza bajeti ya dawa kwa kiasi kikubwa huku mpango wa kuokoa vifo vya akina
Mama wajawazito na watoto wachanga tukilisimamia kwa nguvu zote.. Hii ni sera
yetu na tuendelee kukiunga mkono chama chetu” alieleza Dk. Kigwangalla na kisha alichangia kiasi cha Tsh. 500,000,
kama mchango wake kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya ujenzi huo wa jengo hilo
la CCM Mkoa wa Songwe.
Mbali na
kutembelea ofisi hizo za CCM, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wakukagua
Hospitali ya Vwawa na vituo mbalimbali vya Mkoa huo ikiwemo kituo cha Afya
Mbuyuni na Iyula.
Wakati huo
huo, Dk. Kigwangalla amemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbozi, Eliasey Ngowi
kukamilisha boma la chumba cha upasuaji
linalojengwa katika kituo cha Afya Iyula na ujenzi wake ukamilike ndani ya
miezi mine.
“Nakuagiza
Mkurugenzi boma ili la upasuaji
likamilike ndani ya miezi mine. Na nitakuja hapa kulizindua mimi mwenyewe, ukae
kwenye vikao vyenu huko na kushirikiana na Mbunge wa hapa, wananchi na hao
wahisani muliowapata na mukamilishe haraka sana” alieleza Dk. Kigwangalla.
Aidha,
alipongeza juhudi za watumishi wa sekta ya Afya kwa kuendelea kutoa huduma bora
huku akimwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe kuhakikisha anakamilisha mifumo
ya maji ndani ya chumba cha upasuaji, Maabara na wodi ya Wazazi kwenye
hospitali hiyo ya Vwawa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.