ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 28, 2017

UWEPO WA MAHAKAMA INAYOTEMBEA, ELIMU SAHIHI KWA WAKULIMA, VYALIPAISHA THAMANI ZAO LA PAMBA.

Madereke Kombe ambaye ni Katibu Chama cha Msingi Cha Wakulima wa Kata ya  Mwabusalu wilayani Meatu mkoa wa Simiyu, anasema kuwa mwamko wa wakulima kujitokeza kwa wingi kuuza pamba ni kutokana na kilimo cha mkataba kuonekana kuwa na manufaa kwao. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA

Mfumo umewapatia mazao mengi.
Awali wakulima walikuwa wakilima hekari tano hadi kumi na kupata mazao kiduchu tofauti na ukubwa wa shamba, lakini imekuwa tofauti na sasa wamefanikiwa kuvuna pamba kiasi cha kupiku ulimaji wa kizamani. Mtu anaweza kulima heka mbili tu kwa usahihi bila kuchanganya mazao mengine na kupata mazao ya uhakika mengi kama thamani ya shamba la zamani la hekari tano, haya ni maajabu" Alisema mmoja kati ya wakulima.


Mizani ya pamba.... 
Awali wakulima walikuwa wakiipeleka pamba yao sokoni kwa kuchanganya na takataka na sababu kuu ya kufanya hivyo wanasema ni kutokana na unyanyasaji wa bei pamoja na dhuluma zilizokuwa zikifanywa na wanunuzi wa awali katika mizani.
Irene Marenge ambaye ni Afisa Maendeleo na Uhusiano wa Zao kutoka Bodi ya Pamba Mwanza anasema kuwa tatizo la uchakachuaji kwenye mizani lilikuwa sugu na lenye kuhatarisha maisha ya zao la pamba Kanda ya Ziwa. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.

Uchakachuaji mizani ulisababisha zao letu kukosa ubora kwasababu wanunuzi walikuwa wakifanya ukorofi kwenye mizani na kuwaibia wakulima, wakulima nao walikuwa wakilipa kisasi kwa kuweka maji, mchnga, chumvi na vitu vingine vilivyokuwa vikisababisha ubora wa pamba kushuka lakini kwa kushirikiana na wakala wa vipimo ambao wako chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, Bodi ya Pamba imejipanga kudhibiti tatizo hilo.


Wakulima sasa wanauza pamba bila wasiwasi kabisa kwasababu ya usimamizi unaoendelea chini ya Wasimamizi wa Bodi.
MAHAKAMA INAYOTEMBEA.
Bodi ya Pamba tayari imetangaza Mahakama inayotembea na msimu wa manunuzi na mauzo ikisema kuwa Haitokuwa tena na huruma kwa wale wote iwe wakulima watakao husika na kuchafua pamba kwa kuweka vitu visivyofaa kwenye bidhaa hiyo au wanunuzi watakao kuwa wakinunua pamba kwa kutumia mizani zilizochezewa.

"Hakutakuwa na Huruma kwani tuna mahakama zinazotembea, yeyote ambaye atabainika kutenda kosa hilo atachukuliwa hatua hapo hapo na hukumu kutolewa" anasema Irene Karenge

Kisha akaongeza "Hakuna cha kupeleka mtu tena mahakamani, ushahidi umepatikana kwenye tukio (sokoni) hatua za hukumu zinachukuliwa papo hapo, kama ni kifungo au faini ni papo kwa hapo mtu anaandikiwa hukumu" 

Afisa Maendeleo na Uhusiano wa Zao kutoka Bodi ya Pamba Mwanza Bi. Marenge anatoa rai kwa wakulima kuondoa shaka juu ya soko kwa mazao yao na kuwataka kujitokeza kwa wingi kuuza pamba akisema kuwa na msimu wa kilimo utakapo wadia tena washiriki kwa wingi.
Kazi kazi ndani ya ghala la pamba.
Vipimo kwaajili ya usafirishaji kuelekea kwa
Zao mkononi.
Mkulima akihojiwa pindi alipotembelewa na wanahabari nayo Jembe Fm ikinasa ujumbe wake ni katika ziara ya kutembelea kuona mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba (UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu mkoani Simiyu.
Jicho la Kamera ya Gsengo na unakili sauti wa Jembe Fm linanasa taswira ya zao la pamba ndani ya kata ya Mwabusalu.
Live na mkulima.
Jembe Fm iliangusha sahihi yake hapa ikimaanisha mguu ulitia timu pande hizi za Mwabusalu.
 Kama 'Tomaso' vile nalishika zao.........
Utekelezaji wa Mpango wa uzalishaji wa Mbegu bora katika kata ya Mwabusalu Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu umehusisha jumla ya wakulima 1,709 katika vijiji vinne ambao kwa pamoja wameweza kulima jumla ya ekari 6,506 na unafadhiliwa na Programu ya Kuendeleza Kilimo cha Pamba chini ya usimamizi wa Bodi ya Pamba.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.