ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 2, 2016

WENJE APATA PIGO MAHAKAMANI

ALIYEKUWA mgombea ubunge jimbo la Nyamagana , Ezekia Wenje (Chadema) amepata pigo baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kutupilia mbali maombi aliyowasilisha katika kesi ya kupinga matokeo uchgauzi Mkuu jimboni humo.

Wenje aliyekuwa mbunge wa Nyamagana awamu iliyopita, alifungua kesi namba 5/2015 akipinga matokeo yaliyoangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yakimpa ushindi Mbunge wa sasa, Stanslaus Mabula (CCM).

Pigo hilo amelipata leo, baada ya Jaji Kakusulo Sambo wa Mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya Wenje ya kutaka kutumia fomu ya NEC namba 21B ya matokeo ya vituo vyote 693 vya jimbo hilo ili vikaguliwe upande wa utetezi.

Hata hivyo Wenje aliyepewa muda kufanya hivyo kisheria, alishindwa kutekeleza ndani ya muda na kuomba tena kuongezewa muda, ombi hilo na lile la kutaka Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi (kwa niaba ya NEC) na Mbunge Mabula ambaye ni mlalamikiwa wa pili katika kesi hiyo, wahojiwe kwa maswali yaliyoandikwa, ziligonga mwamba.

“Kutokana na maswali jinsi yalivyo, hutumika kwenye kesi za kawaida hivyo ni vyema utawahoji wakati wa kesi ya msingi itakaposikilizwa,” alisema Jaji Sambo akizingatia kuwa ingeweza kupunguza muda wa usikilizwaji na wingi wa mashahidi.

Jaji huyo alidai kesi ya msingi sasa itaanza kusikilizwa Machi 7 mwaka huu bila kusimama.

Kabla ya kuiahirisha baada ya upande wa Wenje ukiwakilishwa na wakili HEZRON kudai wakili wao kiongozi Dea Outa anaumwa huku uande wa utetezi unao ongozwa na Costantine Mtalemwa nao ukiomba udhuru wa kuhudhuria kwanza Kikao cha Mahakama Kuu ya Rufaa Arusha.

Wafuasi wa Chadema waliokuwa nje ya Mahakama hiyo baada ya kumuona Wenje akitoka na kuwapa salamu ya “Peoples Power”  wanayotumia chama hicho, bila kujua kichoamliwa, walilipuka kwa shangwe na kuanza kuandamana wakidai wameshinda kesi.

Kutokana na hatua hiyo iliyosababisha kelele katika maeneo ya mahakama, polisi walilazimika kuwatawnya katika maeneo hayo na maeneo mengine ya barabara za Nyerere, Pamba na Mlango mmoja ili wasisabaishe uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali za wananchi waliokuwa wakiendelea kuchapa kazi.

Akizungumza baada ya maandamano ya wafuasi wa Chadema, wakili wa Mtaremwa amesema kwa upande wake wa utetezi kitendo cha kutupwa kwa maombi ya mlalamikaji ni hatua muhimu kuelekea kwenye kesi ya msingi hivyo wanaoshangilia wana ‘mahaba’ lakini siyo matakwa ya kisheria aliyotolewa Mahakamani hapo.

Wakili Mtalemwa amewaasa waandishi wa habari na mitandao ya kijamii inayofatilia kesi za uchaguzi kuwa makini na kuzingatia maadili bila kutopotosha umma kwa maslahi binafsikwani tasnia ya habari ni nguzo mhimu inayotegemewa kujenga taifa na jamii katika misingi ya amani na utulivu. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.