Na Peter
Fabian, MWANZA.
MKUU wa
Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Baraka Konisaga, ameamuru Mkurugenzi wa Jiji
la Mwanza, Adam Mgoyi kuwasimamisha kazi madaktari wawili na wauguzi wanne katika
Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana iliyopo Kata ya Butimba kwa kushindwa
kumuhudumia mama mjamzito aliyefikishwa
hospitalini hapo na kusababisha kujivungua watoto mapacha na badae kufariki.
Hatua
hiyo inafuatia tukio la mgonjwa Suzana John (27) mkazi wa Kata ya Mkolani kufikishwa
na ndugu zake katika Hospitali hiyo aliyekuwa mjamzito na kupokelewa na Dr Norin
Magesa na Muuguzi Janet Foya waliokuwa zamu ya usiku siku ya March mosi mwaka
huu majira ya saa 4:00 usiku na kushindwa kumuhudumia zaidi ya kutoa lugha
isiyolizisha ikiwa ni pamoja na uzembe.
Awali DC
Konisaga baada ya kufika Hospitalini hapo juzi majira ya saa 2:45 usiku wa
March 2 mwaka huu na kukutana kwa dhalula na Mkurugenzi wa Jiji, Adamu Mgoyi,
baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Nyamagana, Kaimu Mganga
Mkuu Mkoa,Uongozi wa Hospitali na baadhi ya ndugu wa mgonjwa Suzana John
aliyejifungua watoto mapacha waliokuwa hawajatimiza muda wao (Njiti) kisha
vijanga hivyo kufariki baada ya kukosa huduma.
Katika
kikao hicho cha dhalula kupokea maelezo ya pande mbili kutoka kwa wauguzi na
familia ya mgonjwa Suzana na kupitia taarifa zilizokuwa zimeandikwa na Madaktari
wawili waliomuona mgonjwa huyo ndipo DC Konisaga akamuagiza Mkurugenzi Mgoyi na
Kaimu Mganga Mkuu kuwasimamisha kazi madaktari wawili na wauguzi wanne ili
kupisha uchunguzi wa kitaalamu juu ya tukio hilo.
Konisaga
aliwataja wanaotakiwa kusimamishwa kazi kuwani Dr Magesa na muuguzi Foya
waliompokea mgonjwa wakiwa zamu ya usiku wa March mosi mwaka huu na kushindwa kumpatia
huduma zaidi ya kumtolea lugha chafu na uzembe huku wakishindwa kutoa maelezo
wakati wa kukabidhi kwa majukumu kwa madaktari na wauguzi walioingia zamu ya
asubuhi ya March 2 mwaka huu.
DC
Konisaga pia alieleza kuwa pamoja na kuingia kwa madaktari na wauguzi wa zamu ya
asubuhi ya March 2 bado hawakumjali na kumhudumia mgonjwa huyo huku baadhi
wakitoa lugha zisizo za faraja kwa ndugu wa mgonjwa na hata alipozidiwa na
kupewa taarifa na ndugu wa mgonjwa huyo hawakufika na mara kadhaa walikuwa
wakifika na kutoka bila kumudumia pamoja na kumsikiliza akilalamika.
Aliwataja
wengine wanaotakiwa kusimamishwa kazi mara moja ni Dr Emiliana Mvungi, wauguzi
ni Maria Mkankule, Suzana Sindano na Bibiana Moshi ambao walikuwa zamu na
kutomhudumia mgonjwa ambaye alijifungua katika mazingira hatarishi akiwa
Hospitalini hapo bila kupatiwa huduma hali iliyopelekea kujifungua vichanga mapacha
wakiwa hai lakini walifariki nusu saa baadaye kwa kutopewa huduma.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo alimwagiza Kaimu Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Dr Rweyendela Onesmo ambaye ni Mganga Mkuu Mfawidhi wa
Hospitali ya Mkoa ya Sekou-Toure kupewa maelezo ya kina kutoka kwa Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo,Dr Nangi William na Mganga Mkuu wa Jiji, Dr John
Andereaw juu ya kushindwa kuchukua hatua pamoja na kupewa taarifa hizo.
Mulongo
pia alimuagiza Dr Onesmo kuunda tume ya uchunguzi itakayoshughulikia suala la
tukio hilo na kisha kukamilisha kazi hiyo kwa siku moja na kumpatia taarifa ili
hatua kali za maadili ya utumishi wa umma yachukue mkondo wake huku pia
kuwezesha kusaidia jinsi ya kuboresha utendaji wa kitaalamu na kitabibu katika
Hospitali hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kutokuwa
na huduma nzuri kwa wagonjwa.
Akisimulia
mkasa huo Dada wa mgonjwa Suzana aitwaye Estha John (35) mkazi wa Sengerema
aliyekuwa akimhudumia alieleza kupata wakati mugumu ikiwemo kutolewa lugha za
mauzi na wauguzi huku Daktari akishindwa kufika kwa wakati kuokoa maisha ya
vichanga hivyo na kusababisha uzembe uliopelekea kupoteza maisha pamoja na
kuzaliwa wakiwa na miezi sita sawa na wiki 24 kisha kufariki dunia.
Estha
alisema kwamba vichanga hivyo viwili lilikuwa vya jinsia ya kike na kiume na
tayari kulitokea mabishano makubwa baada ya kufariki kutakiwa kuchukua miili
kwa ajili ya mazishi hali ambayo ilireta kutokuelewana na kusababisha ndugu wa
familia ya mgonjwa ikiongozwa na mume wake Peter Michael (36) mfanyabishara
mkazi wa Mkolani kutaka kupigana huku wananchi nao wakiunga mkono waliokuwa
Hospitalini hapo.
Hali
hiyo ilisababisha kuibuka kwa vurugu kubwa Hospitalini hapo na
kupelekea viashilia vya uvunjifu wa amani na kupelekea DC Konisaga
kufika hapo majira ya saa 2:45 hadi saa 5:45 usiku kufanya mazungumzo ya
kina na familia ya mgonjwa na uongozi wa Jiji, Hospitali kabla ya
kukubaliana kisha kutoa tamko la kusimamishwa kazi kwa madaktari na
wauguzi hao kupisha uchunguzi wa kilichopelekea vifo vya watoto hao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.