Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni
ya PanAfrican Energy Andrew
Kangashaki (kushoto ) na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa
Twalib Mbasha wakikabidhiana mkataba wa miradi ya ujenzi wa nyumba ya mama ngojea katika hospital ya Kinyonga na ukarabati wa wodi ya uzazi mara baada ya kumaliza kusaini mikataba hiyo katika hafla fupi iliyofanyika jana Kilwa Kivinje.
Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Kampuni
ya PanAfrican Energy Andrew
Kangashaki(wa tatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa
Twalib Mbasha (wa tatu kulia) wakisaini makubaliano ya miradi miwili ya ujenzi
wa mama ngojea ‘maternity waiting home’ yaani nyumba maalum kwa kina mama
wajawazito watakaokua wakisubiri kujifungua itakayojengwa katika hospitali ya
Kinyonga – Kilwa Kivinje na kukarabati wodi ya uzazi na chumba maalum cha
uangalizi wa akina mama mara tu baada ya kujifungua katika kituo cha afya cha
Kilwa Masoko. Huku wakishuhudiwa na Mwanasheria wa Wilaya Mh. Godfrey Makary
(wapili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Juma Abdalah Njwayo(wa pili
kushoto), Mbunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia chama cha CUF Mh. Vedasto
Edgar Ngombale(wakwanza kushoto) pamoja na Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama
cha CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wakwanza kulia).
Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha
CUF Selemani Bungawa a.k.a Bwege(wapili kulia) akitoa neno la shukrani kwa
Kampuni ya PanAfrican Energy kwa niaba ya wananchi wa Kilwa Kusini mara baada
ya makabidhiano ya mkataba wa miradi itakayowanufaisha wananchi wa kilwa.
Wafadhili wa mradi wa ujenzi wa wodi ya
wazazi Kampuni ya PanAfrican Energy pamoja wakiwaonesha wanahabari chumba cha
uzazi katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko ambacho kipo katika mradi uliosainiwa
kati ya wilaya ya Kilwa na kampuni hiyo. Hii ni katika kuunga jitihada za
serikali za kuboresha huduma za afya.
Hali
halisi ya mazingira ya wodi ya wagonjwa katika kituo cha afya cha Kilwa Masoko,
hii ni wodi ya wanaume. Kiyuo hichi cha afya
kilijengwa mwaka 1952 enzi za ukoloni mpaka sasa hakijawahi
kukarabatiwa.
Wakisaini makubaliano ya miradi ya ujenzi
wa mama ngojea na ukarabati wa chumba cha uzazi na wodi maalum ya uangalizi wa
kina mama mara tu baada ya kujifungua wilayani Kilwa ni Meneja Uwajibikaji kwa
jamii kutoka Kampuni ya PanAfrican Energy Andrew Kangashaki(wa pili kushoto)
pamoja na Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Twalib Mbasha (wa pili kulia)
wanaowashuhudiwa ni Mwanasheria wa Wilaya ya Kilwa Mh. Godfrey Makary ( kulia),
Mkuu wa Wilaya ya hiyo Juma Abdalah Njwayo (kushoto) jana katika hafla fupi
iliyofanyika jana katika hospitali ya Kinyonga Kilwa Kivinje.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.