Ni muda wa kazi sasa .....
Naaam mara baada ya shughuli za usafi tangu asubuhi mpaka sasa ambapo sisi kama Jembe Fm na wadhamini wetu pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi mkoa wa Mwanza tumeweza kujumuika pamoja na kufanya shughuli za usafi katika hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Naomba sasa kwa niaba ya mkurugenzi wa Jembe Media Group Bw. Sebastian Ndege, inakuwa ni vyema kutoa shukurani kwa wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wameweza kushiriki nasi kutimiza azma yetu kuweza kushiriki kikamilifu maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) katika shughuli za usafi kama ilivyoamriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.
Ambapo sisi kama Jembe Media Group tulijipanga kufanya usafi madhubuti kwa hospitali yetu ya mkoa Sekou Toure ...Na kweli Tumelitimiza hilo.
Tunatambua mchango wa wadau mbalimbali toka wilaya mbalimbali zinazo uzunguka mkoa wa Mwanza kwa kushiriki nasi kwenye zoezi hili la usafi kwa kuzihudumia hospitali zenu za wilayani mwenu, sanjari na mazingira ya majumbani mwenu.
Naam hilo ndilo lilikuwa kusudio letu.
Shukurani za dhati ziwaendee wadau mbalimbali waliotoa ushirikiano na ushauri kwetu tukiwa na imani kuwa zoezi hili litakuwa endelevu na la kudumu.
Wacha ninukuu kauli ya Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula "Tunataka kuifanya siku hii ya Uhuru iwe kama ufunguo wa Usafi wa kudumu kwa mazingira ya kaya zetu na Taifa kwa ujumla" mwisho wa kunukuu.
Aksante tena na tena kwa Makampuni yaliyo tushika mkono na kuungana nasi Kampuni ya vifaa vya solar MOBISOL, STARTIMES, BOA BANK, TBL Mwanza, WAJASILIAMALI KWANZA, wakuu mbalimbali wa Serikali kuanzia Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana Raphael Shilatu, Mganga mkuu na msaidizi wa Hospitali ya Sekou Toure, wakunga na wauguzi wote wa hospitali hiyo pamoja na wale wote walioonyesha nia ya kushiriki nasi lakini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao wakashindwa kujumuika nasi.
Tunaimani kuwa hatutoishia hapa tu, mtashirikiana nasi katika makubwa mengine yaliyo mbele yetu.
HAPA KAZI TU.
Mungu ibariki Afrika,
Mungu ibariki Tanzania.
#JEMBEFAMILY @jembenijembe
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.