AIRTEL FURSA YATUA BUKOBA, YAONGEA NA VIJANA KUTOOGOPA VIKWAZO KATIKA UJASILIAMALI ·
Bukoba zaidi ya wajasiliamali vijana 200 wanolewa na Airtel Fursa Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi airtel imewataka watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwa kufanya ujasiriamali kwa mtazamo mpana kwa lengo la kuondokana na umasikini au maisha duni yasiyo na kipato maalum.
Hayo yamesemwa na mwalimu wa mambo ya ujasiliamali ambae pia ni Afisa ujasilimali wa VETA mjini bukoba Bw, Frabius Ngemela kwa zaidi ya wajasiliamali 200 waliohuduria semina ya ujasiliamali ya Airtel Fursa BUKOBA akiwataka vijana wajasiliamali kutumia ujuzi na maarifa katika kuboresha miradi yao kama njia mojawapo ya kukabiliana na suala la umasikini na kuwataka wajasiliamali hao kutokata tamaa ya maisha badala yake waongeze juhudi katika uzalishaji mali bila kuogopa vikwazo ili kujikomboa.
Airtel Fursa imekuja Bukoba leo kuwaambia msikate tamaa, nawafundisha leo kuvitambua vikwazo na msiviogope katika shughuli zenu, mkashirikiane na mradi wa Airtel Fursa ili kujikwamua.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alieleza “Airtel Fursa sio tu tunawasaidia vijana kuzitambua fursa pia tunawapatia mitaji na vitendea kazi muhimu ambavyo vimekua ni vikwazo vya kutimiza malengo yako ili uweze kuzalisha zaidi na kusaidia jamii zao
“Hadi sasa tumeshazunguka mikoa zaidi ya 12 ndani ya miezi hii minne tukiwaeleza vijana jinsi wanavyoweza kukamata FURSA na kuwasaidia kupitia warsha kama hizi pia kuwapatia vitendea kuza lishakazi na vifaa mbalimbali waweze kuzalisha zaidi” alisema Mmbando wakiongea mara baada ya kupatiwa elimu ya ujasilimali baadhi ya wajasiliamali wadogo Peace Ruben MJASIRIAMALI,
Alisema licha ya kupatiwa elimu hiyo bado wanakabilina na changamoto mbalimbali ikiwemo mitaji ya kuendeshea biashara zao ambapo pia wametumia nafasi hiyo kuiomba kampuni ya airtel kwa kutumia mradio wao wa Airtel fursa kuwapatia mitaji itakayo wasaidia kuendesha biashara zao.
“Mi kazi yangu ni kufuma vitambaa na nguo za kuzuia baridi kwa watoto , wateja wangu wanapatikana kwa urahisi hapa bukoba na nje ya bukoba yaani hapo mpakani mwa Tanzania na Uganda lakini tatizo ni vitendea kazi vya kutosha ili kuongeza uzalishaji, ikiwa Airtel Fursa itanitoa nitafurahi sana” alieza Peace Ruben.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.