ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 21, 2015

KAHAMA YAONGOZA KWA MAAMBIKIZI YA UKIMWI KITAIFA.

Imeelezwa kuwa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga inaongoza kwa maambukizi ya UKIMWI kwa kiwango cha asilimia 5.5 zaidi ya kiwango cha kitaifa ambacho ni asilimia 5.1.

Hayo yamesemwa leo na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya alipokuwa akisoma taarifa ya maambukizi ya UKIMWI kiwilaya katika hitimisho la mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo.

Mpesya anesema kiwango hicho kimeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana ambapo maambukizi yalikuwa asilimia 4.8 hali ambayo imedaiwa kusababishwa na watu wengi wilayani humo kutofuata njia za kujikinga na maambukizi hayo.

Aidha Mpesya anesema maambukizi yanaongezeka kwa kasi kutokana na mwingiliano wa watu wengi katika wilaya ya Kahama ambayo inafursa nyingi za kibiashara hali inayopelekea elimu inayohusu maambukizi ya UKIMWI kutofanikiwa kutokana na mwingiliano huo.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu Juma Khatibu amewataka wananchi wilayani humo kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya UKIMWI kwani kiwango hicho kinaonesha kuwepo kwa kasi kubwa ya maambukizi wilayani humo.

Ameongeza kuwa njia pekee ya kuepusha kasi ya maambukizi hayo ni wananchi kupima virusi ili kujua afya zao na kufuata njia sahihi za matibabu ya ugonjwa huo na wakijitambua wasiwaambukize wengine maksudi.

Mwenge wa Uhuru leo umekabidhiwa Manispaa ya Shinyanga ukitokea wilaya ya Kahama ambapo kaulimbiu yake mwaka huu"Tumia haki yako kupiga kura 2015, kidemokrasia jiandikishe katika daftari la kudumu la mpiga kura".

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.