ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 17, 2014

WAANDISHI WA HABARI MWANZA WAPIGWA MSASA KUISAIDIA JAMII KATIKA MAAMUZI YA KISHERIA.

Jimmy Luhende ni Mmoja kati ya waendesha warsha ambao walisimamakidete hii leo kutoa elimu kwa waandishi wa habari mkoani Mwanza inayohusu Usaidizi wa Sheria kwa jamii, iliyoanza leo katika ukumbi wa VETA Igoma jijini Mwanza. 
Washiriki nao walipata fursa ya kuchangia ili kupimwa uwezo na uelewa wao. ambapo dhana za mijadala mbalimbali ziliwakilishwa na kujadiliwa kama vile :- Ufahamu wa Sheria, Ndoa, Nini maana ya Rehani, Talaka, Mirathi na kadhalika.
Usaidizi wa Kisheria ni nini?
Huyu ni mtu mwenye ufahamu wa sheria na masuala ya haki, mwenye kuweza kushauri na kuelekeza jamii kufuatilia haki katika vyombo vya sheria na vya haki.

Yeye si mwanasheria kifani wala si wakili bali ni mtoa huduma za sheria kwa jamii na mfuatiliaji wa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa umakiiini ni Nashon Kennedy wa Habari Leo (L) na Albert G. Sengo wa Clouds Media (R). 
Matarajio na Malengo ya warsha:
. Kuwezesha washiriki kuongeza uelewa kuhusu ukiukwaji wa haki na usaidizi wa sheria nchini Tanzania.
. Kuwawezesha washiriki kuripoti masuala mbalimbali kwa ufasaha hasa yale yanayo husisha uelewa wa sheria.  
WARSHA HII INASIMAMIWA NA SHIRIKA LA KIVULINI MWANZA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.