Press Release
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imekabithi waandaaji wa Tuzo za mwanamakuka The Unity of Women Friends kiasi cha million tano pesa taslimu wakati wa halfa ya tuzo za mwanamakuka 2014 zilizofanyika jijini Dar es saalam mwisho wa wiki
Tuzo hizi za mwanamakuka 2014 ziliwashirikiasha washindi 10 wa mwaka 2012 na mwaka 2013 ambapo washindi hawa walifatiliwa biashara zao na kuchaguliwa mshindi mmoja aliyefanya vizuri na kutumia vyema zawadi aliyoshinda katika kuendeleza biashara zao ambapo bi Leila Mwambungu aliyekuwa mshindi wa pili mwaka Jana kuibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014
Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema” Tunayofuraha kuwa wadhamini wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa miaka mitatu mfululizo kwa sasa na kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko kwa wanawake kupitia tuzo hizi. tunafurahi kuona jinsi kina mama hawa wajasiriamali walioshinda miaka iliyopita wakifanya vizuri katika biashara zao.
Na sisi Airtel leo tunakabithi kiasi cha kiasi cha shilingi milioni tano kama mchango wetu kwa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka 2014. Tunaamini kiasi hichi cha fedha kitaweza kuwawezesha waaandawaji wa tuzo hizi kufanikisha halfa hii na kuwafikia wanawake na kuwawezesha kutanua mitaji yao na hatimae kuongeza kipato na faida zaidi na kujikwamua kiuchumi”.
“Tutaendelea kushirikiana na The unity of Women Friends ili kuhakikisha tunaweza kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini” aliongeza Matinde.
Kwa upande wake mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu Alisema “naona fahari na furaha kuwa mshindi wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka huu, napenda kuwashukuru sana waandaaji wa tuzo hizi kwa kuniona kupitia juhudi ninazoziweka katika kazi zangu na biashara zangu. Mpaka sasa nimeweza kuajiri watanzania kupitia biashara zangu na Kiasi hii nilichozawadiwa leo kitanisaidia sana kukuza mtaji. Cha msingi wanawake tupendane na kushirikiana napenda kuwahasa wanawake wenzangu kutokata tamaa na kuongeza katika biashara zao, haijalishi kama mtaji mdogo bali wajipange na kujikita katika uzalishaji na hatimae kuinua mtaji na kuweza kufanya biasha kwa mtaji mkubwa, hakuna siri nyingine ya mafanikio zaidi ya jitihada , hari na kujiwekea malengo na kuhakikisha yanafikiwa kwa wakati uliopagwa.
Naye mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo alisema Tuzo hizi za Mwanamakuka zinaendelea kukua na kuziboresha zaidi, kwa mwaka huu lengo letu lilikuwa ni kuwawezesha wachache kwa kuwafatilia washindi wetu 10 wamiaka iliyopita na kuona jinsi gani biashara zao zinavyoenda na kumzawadia anayefanya vizuri zaidi. Lengo ni kuendelea kuwahamasisha na kufatilia mafanikio yao kwa karibu.
Vilevule tukiangalia miaka iliyopita tuliweza kuwashirikisha wanawake tu katika sherehe za tuzo hizi lakini kwa mwaka huu tumeamua kushirikisha familia kwa kuandaa bonanza ambapo wakinababa na watoto kwa pamoja tunasherehekea mafanikio haya, na kusherehekea siku ya wanawake duaniani huku tukienzi juhudi za wanawake jasiri nchini na kuwazawadia
Tunashukuru sana Airtel kwa kushirikiana nasi miaka mitatu kwa sasa na tunaamini kuwa bado wataendelea kutoa mchango wao na kushirikiana nasi na kutuunga mkono kwa miaka mengine ijayo na kuhakikisha lengo letu la kumwinua mwanamke wa kitanzania linafikiwa. Alisema Shamo
Kwa mwaka huu Tuzo hizi zilishirikisha washindi waliopatikana miaka iliyopita ambapo kati yao pamoja na Tatu Ngao, Mwananne Msekalile, Sikudhani Daudi, Nasra, Aziz, Khalid, Leila Mwambungu, Selestina Renatus, Maajab Yusufu na Agnes Daudi ambapo Bi Leila Mwambungu Ameibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.