ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 7, 2013

WADAU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MWANZA (MPC) WAJITOKEZA KUCHANGIA UNUNUZI WA MASHINE YA KUCHAPISHA MAJARIDA

Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Mwanza (MPC) Deus Bugailwa akitamka ahadi za watu mbalimbali na mashirika ambayo hayakufanikiwa kufika katika Harambee hatua ya Mwanza ya kuchangisha fedha ili kununua mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti mbele yake ni Rais wa UTPC Keneth Simbaya. Harambee hiyo ilifanyika katika ukumbi wa JB Belmont Mwanza.

Meneja wa Kanda wa Benki ya NMB Straton Chilongola (wa pili kulia) akiwa na Meneja Mawasiliano wa benki hiyo Bi. Josephine Kulwa wakikabidhi hundi ya shilingi milioni mbili kwa Rais wa UTPC Keneth Mbaya, katika kuchangia harambee ya ununuzi wa mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti. Kushoto kabisa ni Mwenyekiti wa MPC Deus Bugailwa.  

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula alitoa kauli ya ofisi yake kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja kwenye harambee ya ununuzi wa mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti, iliyofanyika Hotel JB Belmount Mwanza.

Ni mkono wa shukurani kutoka kwa mwenyekiti wa MPC Bw. Deus Bugahilwa kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula. Hata hivyo meya huyo hakukaa sana kwenye harambee hiyo kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ya kijamii, hivyo aliomba radhi na kuondoka. 

Ilikuwa ni zamu ya Brother kutoka Mwananchi Communication Fredrick Katulanda.

Na hapa ilikuwa ni zamu ya mdau kutoka New Habari Cooperation Grace Chilongola.

Brother Jimmy Luhende hakulichukulia suala hili mzaa alikuja na mpunga wa kutosha wa kitu 'cash'.

Mwanasheria wa Kampuni ya vyombo vya usafiri majini Marine service hakuwaangusha wanahabari.

Naye katibu wa MPC alihusika changizoni.

Meza ya Mwandishi wa habari wa ITV Mwanza Mabere Makubi ilipendeza sana.

CEO wa Gsengo blog Mr. Albert G. Sengo akiwasilisha mchango wake katika harambee ya kuchangisha fedha ili kununua mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti.

Mahesabu yakifanyika kupata idadi na kiasi kilichopatikana kwani kuna wadau wengine walichangia kwa njia ya mitandao huku tukio likiruka live kupitia Barmedaz Tv.

Kutoka kushoto ni G. Sengo, Grace Chilongola na Mary Ngoboko.

Salaam za kutakiana mema katika safari hii ya harambee hatua ya kwanza kutoka kushoto ni Meneja wa Club Fusion Mwanza Mr. George, Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula, Mwenyekiti wa MPC Deus Bugahilwa pamoja na Rais wa UTPC Keneth Simbaya.

Mie, George Ramadhan wa IPP na mwanahabari Mc Chonya ambaye kwa hivi sasa kahamia mkoani Tabora.

Pichani ni Kamati ya Harambee hiyo kutoka kushoto ni George Ramadhani, Deus Bugahilwa, Adventina Kashalaba, Denis Mpagaze, Jimmy luhende, Grace Chilongola, Rais wa UTPC Keneth Simbaya, Kelvin Jilala na Rose Jackob.

Jumla ya shilingi milioni 29,120,000/= zimepatikana kwenye Harambee hii ya kwanza ya kuchangia fedha za kununua mashine ya kuchapisha magazeti kwa Chama cha waandishi wa habari Mwanza (MPC), ikiwa ni safari ya kuelekea  kufikia lengo la kufikisha kiasi cha shilingi milioni 100.  

Tupe maoni yako

3 comments:

  1. I'm curious to find out what blog system you are utilizing? I'm having
    some minor security problems with my latest blog and I
    would like to find something more safeguarded. Do you have any suggestions?


    Feel free to surf to my webpage: World Of Tanks Hack

    ReplyDelete
  2. Thanks for finally talking about > "WADAU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MWANZA (MPC) WAJITOKEZA KUCHANGIA UNUNUZI WA MASHINE YA KUCHAPISHA MAJARIDA" < Liked it!

    Stop by my site - download 7zip

    ReplyDelete
  3. After looking into a handful of the blog posts on your site, I honestly appreciate your way of
    writing a blog. I saved it to my bookmark webpage list and will be checking back in the near future.
    Take a look at my web site too and tell me your opinion.


    My web site: Minecraft Crack

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.