ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 27, 2012

PICHA ZA DR. ULIMBOKA MARA BAADA YA KUOKOTWA AKIWA HOI

Hii Picha halisi ya kiongozi wa mgomo wa madaktari nchini Tanzania dr. Steven Ulimboka akiwa na majeraha baada ya kukamatwa jana usiku nyumbani kwake na watu wasiojulikana na leo asubuhi kukutwa maeneo ya Bunju jijini Dar es Salaam akiwa hoi.
Dr. ulimboka akipelekwa hospitali mara baada ya kuokotwa akiwa hoi
Mmoja kati ya madaktari wenzake amethibitisha kwa lililomtokea daktari huyo na kusema kuwa kwa hivi sasa anaendelea namatibabu licha ya kuwepo kwa taarifa zinazo pishana kuhusu nani wahisika wa kichapo hicho alichopatiwa... kuwa ni watu waliomteka kwa kusingizia kuwa ni maafisa wa jeshi la polisi au ni polisi kweli kweli... 


Dr. Ulimboka prt 2.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kupitia ukurasa wake wa Facebook imeweka picha ya kwanza ya Dr. Ulimboka baada ya kuokotwa akiwa amepigwa vibaya.
"A team from LHRC is making a close follow up of an incident where a defender was kidnapped under a gun point and brutally bitten due to his stance on fighting for the Doctors’ rights. The defender, Dr. Ulimboka is currently in a critical condition, admitted at MOI as he is seen on the picture below, when he was collected from Bunju Police Post at around 10:00 a.m."

Tupe maoni yako

9 comments:

  1. wala haitasaidia kusitisha mgomo kama mambo yenyewe ndo haya

    ReplyDelete
  2. nahisi na macho wamemtoa hatari sana

    ReplyDelete
  3. Mikuki mtamu kwa wagongwa lakini mchungu kwa ulimboka, je hivi ulivyo na maumivu makali halafu unaambiwa madactari wamegoma hivyo huwezi kutibiwa utajisikiaje?????

    ReplyDelete
  4. huyo Dr inatakiwa aachwe hivyohivyo ili aone nn maana ya mgomo

    ReplyDelete
  5. insha mng atamuafuuuuu......

    ReplyDelete
  6. semeni kila mtalo sema ,haya hakuna wakulaumiwa ni wananchi ndio wanaostahili kubeba lawama,kwa kuchagua bora viongozi ili mradi atoke ccm, leo kwa ulimboka kesho kwa nani?
    Michezo hii michafu ya kutoana roho watanzania tulikuwa tunaisikia ,sasa imetua kikamilifu tanzania,subirini hamtoacha kuona rangi, pale ikifika siku sanduku la kura litakapo toa majibu mafisadi wameshindwa ndio mtawajua ni kina nani hao wanaothubutu kutaka kutoa roho za watu kwa sababu eti anapigania haki za watu, muulizeni kubenea mwenye siri nzito kwa yaliyomkuta,mpaka leo hafungui mdomo kumtaja aliyehusika na anamjua waziwazi.

    ReplyDelete
  7. Tunawalazimisha madaktari kufanya kazi, huduma zikiwa mbovu tusilalamike, wabunge wao wanajipangia posho, wengine wamesahaulika na wananchi wanapiga makofi :KIDUMU CHAMA CHA MAFISADI

    ReplyDelete
  8. kwa hili nadhani ni busara kulizungumzia sio siasa, kwa nchi kama ya Tanzania hiki sio kitendo cha kuleta mzaha kumbuka kama angekuwa ni mmoja katika familia yako?? jamani Ulimboka ni mtanzania mwenzetu hakustahili kufanyiwa hivyo hiki ni kitendo cha kinyama

    ReplyDelete
  9. MUNGU NDIYE MWENYE HAKI, WALIOMFANYIA VILE HAWATADUMU MILELE, WATAWAJIBIKA KWA HAKI MBELE YA MUUMBA. ULIMBOKA ALIKUWA AKIONGOZA KULETA MAGEUZI AMBAYO KWA WAKATI HUO YALIKUWA NA GHARAMA KUBWA (SHIDA KWA WAGONJWA)LKN YENYE TIJA KWA TANZANIA IJAYO.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.