ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 22, 2012

KIGWANGALA AUNGANA NA VIGOGO WA CCM MKOA WA MWANZA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU MWANZA

ZOEZI la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania nafasi za uongozi wa juu ngazi ya Taifa na Mkoa kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) umea nza kwa kishindo Mkoani Mwanza kwa baadhi ya vigo go wa chama hicho kikuu cha siasa nchini  kuchukua na kurejesha baaada ya kuanza kwa zoezi hilo rasmi leo Agosti 22 mwaka huu.



Mwenyekiti wa CCM Mwanza Clement Mabina (kushoto) akirejesha fomu kwa mpokeaji Zubeda Mbarouk ambaye ni Katibu Sekretarieti na Maadili Mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya vigogo hao waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya mwenyekiti wa Mkoa wa Mwanza ni Clement Mabina anayetetea nafasi hiyo ambaye amechukua majira ya saa 2:00 asubuhi na kurejesha saa 5:00 asubuhi ,Athon Dialo aliyekuwa mjumbe wa NEC Mkoa wa Mwanza ambaye  amechukua fomu saa 2:30 asubuhi kuwania Uenyekiti, Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor anayetetea nafasi yake ya Katibu wa Uchumi na Fedha naye aliweza kuchukua saa 2:35 .
Mwenyekiti wa CCM Mwanza Clement Mabina (kushoto) akiweka saini kuthibitisha kuwa amerejesha fomu kwa mpokeaji Bi. Zubeda Mbarouk ambaye ni Katibu Sekretarieti na Maadili Mkoa wa Mwanza.


Mwenyekiti wa Mkoa wa Mwanza Clement Mabina anayetetea nafasi hiyo kwa mara nyingine tena hapa anashukuru wanachama wenzake kwa muda alikitumikia chama na akiomba ridhaa yao kwa kipindi kingine kijacho (Bofya play kumsikiliza)


Mbunge wa Nzega mkoani Tabora Dr. Hamisi kigwangala akirejesha fomu kwa Bi. Habiba Haji ambaye ni Katibu Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Mwanza.

Naye Mbunge wa Jimbo la Nzega Mkoani Tabora Dr Hamisi Kigwangala aliyechukua fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa wazazi Taifa majira ya saa 5:20 asubuhi ameamua kuchukuwa fomu yake Mkoani mwanza akiwa safarini kuelekea jimboni kwake huku wanachama wengine wakitajwa kuchukua wakati wowote kutokana na kuonyesha nia ya kuwania nafsai hizo za juu za uongozi wa mkoa na taifa.
Kigwangala akitoa sababu za kugombea nafasi ya Uenyekiti wa wazazi Taifa (Bofya play)
SWALI:- Hudhani kwamba bado wewe u-kijana kuomba uongozi kwenye Jumuiya ya Wazazi yenye taswira ya kukusanya watu waliokula chumvi nyingi? (Bofya play)


SWALI:- Unachukuwa fomu kugombea nafasi ya juu kwa upande wa wazazi wakati ambapo chama kinakabiliwa na changamoto kubwa sana kwa mapokezi yake kwa wananchi, kwamba kimepoteza mvuto ukilinganisha na miaka ya nyuma, kikubwa kikitajwa kuwa chama kimeshindwa kujipambanua kama miaka ya nyuma kilivyokuwa Chama cha wakulima na wafanyakazi wazalendo wa nchi hii miaka ya sasa kinatajwa kuwa kimekuwa kama chama cha kundi fulani la watu, unauambia nini Umma wa Watanzania. (Bofya play)

SWALI:- Kwanini umeamua kuchukuwa fomu Mwanza ile hali wewe ni mwakilishi wa mkoa wa Tabora kama Mbunge? (Bofya play)



SWALI:- Umeanza safari ya kusaka uongozi ndani ya jumuiya ya wazazi nafasi ya uenyekiti lakini Chama kinaonekana kuwa na mipasuko mingi ukipata nafasi uliyoiomba utakisaidiaje Chama cha mapinduzi kuepuka mipasuko? (Bofya play)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.