Wakati
shughuli za uokozi zikiwa zingali zinaendelea, mkuu wa shughuli hizo
Seneh Dumbuya amesema wanakabiliwa na uhaba wa sehemu za kuhifadhia
maiti.
Mkuu wa Mochari
Owiz Koroma amesema wanajaribu kuharakisha kazi za kuhesabu,
kutenganisha na kuzifanyia uchunguzi maiti na kutoa vibali vya vifo
kabla ya shughuli za mazishi.
Ili kupunguza
mbinyo unaozikabili sehemu za kuhifadhia maiti, mamlaka husika na
mashirika ya misaada yanaandaa kufanya shughuli za mazishi kwenye mava
nne tofauti katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown.
Kwa mujibu wa
msemaji wa serikali Cornelius Deveaux mazishi ya watu waliofariki kwenye
janga hilo la maumbile ambalo limetajwa kuwa kubwa zaidi kuwahi
kulikumba bara la Afrika katika miaka ya hivi karibuni yatafanyika kesho
Alkhamisi.
Shughuli za uokozi zikiwa zinaendele.
Wakati huohuo msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekeundu nchini Sierra
Leone Abu Bakarr Tarawallie amesema watu wasiopungua 3,000 wamebaki bila
makaazi na wanahitajia hifadhi, misaada ya tiba na chakula. Kwa mujibu
wa shirika hilo hadi sasa watu wengine 600 hawajulikani waliko.Shughuli za uokozi zikiwa zinaendele.
Rais Ernest Bai
Koroma wa Sierra Leone ameomba misaada ya kimataifa kwa ajili ya wahanga
wa maafa ya maporomoko ya udongo sambamba na kutoa wito kwa wakazi wa
mji wa Regent na wa maeneo mengine yaliyoathiriwa na mafuriko kuhama
haraka iwezekakanvyo ili kutoa fursa kwa jeshi na wafanyakazi wengine wa
huduma za uokoaji kuendelea kutafuta manusura ambao huenda wakawa
wamefunikwa chini ya udongo
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.