Press Release
AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE ZA SEKONDARI MBEYA
Kampuni ya simu ya Airtel chini ya mradi wa shule yetu imetoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya takriban shilingi milioni 2 kwa shule ya sekondari ya Mbeya.
Makadhiano ya vitabu yameshuhudiwa na jumuiya nzima ya Shule yenye zaidi ya watu takribani 1365 wakiwemo wanafunzi, walimu na wafanyakazi wengine waliokusanyika kwa shauku ya kupokea vitabu hivyo ikichagizwa na kauli mbiu ya Airtel Baba lao.
Afisa Masoko wa kampuni hiyo Kanda ya Kusini, Jonas Mmbaga amesema “lengo la kutoa msaada huo ni kutekeleza azma ya kuendeleza ushirikiano na jamii katika Nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ili kukuza taaluma mashuleni. Chini ya mpango wa shule yetu tumeweza kuzifikia shule mbalimbali nchini na leo tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari mbeya.
Mbaga alisema Vitabu hivi ni vya masomo ya sayansi vikiwemo vya Hisabati, Kemia, Fizikia, na Biolojia, kwa ajili ya kidato cha kwanza hadi cha nne. Na tumeichagua shule ya Sekondari Mbeya ili kuwakilisha shule nyingine zilizopo mkoani Mbeya.
“Tunaahidi kuendelea kuzifikia shule nyingi zaidi mkoani hapa na mikoa ya jirani kupitia mpango wetu maalum wa shule yetu ambao ni endelevu uliodumu zaidi ya miaka 7 mpaka sasa. Tuaamini kwa kujikita kwenye sekta ya elimu tunaendeleza ushirikaino wetu na serikali chini ya wizara ya elimu kusaidia kutatua changamoto zilizopo husasani ya vitabu mashuleni na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini”.aliongoza Mmbaga
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari ya Mbeya Bi Magreth Haule alisema” Nawashukuru sana Airtel kwa msaada wa vitabu walioutoa shuleni hapa huu ni uthibitisho kuwa Airtel wapo karibu na jamii hasa katika kuendeleza sekta ya elimu. Msaada huu ni mchango mkubwa na ni changamoto kwa wanafunzi na walimu kuongeza juhudi katika kuhakikisha tunakuza kiwango cha elimu shuleni hapa. Tunaahidi kuvitumia vizuri vitabu hivi kwa manufaa ya wanafunzi na jamii nzima kwa ujumla
Nao Wanafunzi Revina Florence, Denis Michael na Happy Mwaisengela kwa nyakati tofauti na kwa niaba ya wenzao wameipomgeza kampuni ya simu ya Airtel kwa msaada huo na kwamba vitabu hivyo vitachochea hamasa za wanafunzi kuongeza bidii katika masomo ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Vitabu hivyo ni mwendelezo wa shughuli za huduma kwa jamii zinazotelewa na Airtel kupitia mradi maalumu wa Shule yetu unaoziwezesha shule mbalimbali kutapa vitabu vya ada na kiada, mpaka sasa shule zaidi ya 900 zimeshafaidika na mpango huu
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.