NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
TIMU ya mchezo wa pool table ya Kiluvya ‘A’ imeweza kutawazwa mabingwa baada ya kuwafunga wapinzani wao timu ya Maisha Plus kwa seti 4-0 katika mchezo wa fainali wa michuano ya kuwania Ng’ombe mnyama.
Katika fainali hiyo ambayo iliweza kuvuta hisia za mashabiki waliofurika katika ukumbi wa msiaha Plus kutokana nawachezaji wa timu zote mbili kuweza kuonyesha ufundi wa hali ya juu katika kuzigonga kete ili kuweza kuibuka na ushindi.
Kwa ushindi huo timu ya Kiluvya A iliweza kuwa ndio bingwa katika mashindano hayo ambayo yaliandaliwa maalumu kwa ajili ya kuweza kukuza vipaji vya wachezaji wa mchezo huo katika Wilaya ya Kibaha na maeneo mengine ya jirani.
Kikosi hicho cha timu ya Kiluvya ambacho kilikuwa kinaundwa na wachezaji saba kiliweza kukabidhiwa zawadi hiyo ya Ng’ombe mnyama pamoja na jezi, huku nafasi ya mshindi wa pili ambao ni timu ya maisha plus wakinyinyakulia zawadi ya mbuzi.
Katika michuano hiyo nafasi ya mshindi wa tatu ilikwenda kwa vijana wa timu ya Kontena bar ambao waliweza kuzawadiwa jezi, huku nafasi ya mshindi wan ne ikinyakuliwa na timu kutoka maeneo ya Kwa mathias amabao nao waliweza kuonyesha ushindani mkuwa katika hatua ya nusu fainali licha ya kuondolewa.
Kwa upande wake Mkuu wa jeshi la polisi Wilaya ya Kibaha Claurence Mwenda amewataka wachezaji kuachana na tabia ya kupoteza muda mwingi kwa kukaa vijweni na badala yake wahakikishe wanajikita zaidi katika kushiriki katika michezo mbali mbali kwani ni moja ya fursa ya kupata ajira.
Mwenda alisema kwamba kuna baadhi ya vijana wengine wamekuwa wakitumia madawa ya kulevya kitu ambacho amedai kinasababbisha kumaliza nguvu kazi ya taifa, hivyo amewasihi waachane kabisa na matumizi hayo, na kuangalia ni njia gani mbadala wanaweza kuitumia katika kujipatia kipato kupitia sekta ya michezo.
“Mchezo wa pool kwa kweli ni mzuri na mimi nimeweza kushihudia mashindano hayo kwa kweli timu zote zieweza kucheza kwa ufundi mkubwa lakini siku zote ni lazima kuwa na mshindi ambaye hatapatikana, lakini rai yangu kubwa mchezo huu msiutumia vibaya maana wengine wanautumia kwa njia ya kamali kitu ambacho sio kizuri na Rais ameshakataza kucheza mchezo wa pool wakati wa kazi,”alisema Mwenda.
MICHUANO hiyo ya mchezo wa pool ambayo ilizishirikisha timu nane kutoka maeneo mbali mbali yaliandaliwa na ofisi ya Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani kwa lengo ya kuweza kufufua na kuibua vipaji kwa vijana katika mchezo huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.