Tanesco fraudsters to end up in court
By MIKE MANDE The EastAfrican
Posted Saturday, November 24 2012 at 15:08
Posted Saturday, November 24 2012 at 15:08
IN SUMMARY
- A report of a forensic audit at the Tanzania Electric Supply Company Ltd (Tanesco) was handed to the government last week, with the recommendation that those involved be brought to justice.
- The investigation revealed multiple cases of suspected fraud in procurement of goods.
Gazeti hili limenukuu
taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller
and Auditor General). Taarifa hiyo inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi
yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia
manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL.
Itakumbukwa kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo
lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge
ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za
ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa
manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit).
Katika mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza
swali Bungeni kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa
IPTL na baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya
Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii. Kamati ya Nishati na
Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu January Makamba ililitaka Bunge
kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hili kwenye Taarifa yake ya mwaka
2011 iliyowasilishwa Bungeni mwezi Aprili mwaka 2012. Waziri Kivuli wa Nishati
na Madini ndugu John Mnyika katika Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka
2011 alipendekeza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote
hizo hazikuzaa matunda.
Kipindi hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi
bilioni 15 tu. Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye
taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86.
Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa
zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi.
Hivi sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya
kuendesha mitambo ya umeme. Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo kutoka
TANESCO.
Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila
mwezi kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, Taarifa za
kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina cha maji chini ya
kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 tu ya uwezo
(installed capacity). Iwapo TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo
Mtera, Mitambo itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo
kuu ya Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama
wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha Maji
kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha maji.
Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika
sekta ndogo ya umeme hapa nchini;
1. Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya
umeme wa dharura iwekwe wazi na ‘racket’ inayosemekana kuiba jumla ya shilingi
bilioni 86 ionyeshwe na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila
kuchelewa.
2. Waziri wa Nishati na Maadini
auleze umma hali yalisi ya sekta ya umeme nchini, uzalishaji wa umeme upoje,
hali ya maji katika bwawa mkakati la Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL,
kesi zake na utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii
zimalizwe nje ya mahakama. Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme
unakwisha lini maana muda uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari
umekamilika. Waziri aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na
CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa shilingi bilioni
86 za kununua mafuta ya IPTL.
3. Waziri wa Fedha na Uchumi
aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina imetoa kununua mafuta ya
kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Mwezi Novemba mwaka 2011 na
Oktoba mwaka 2012 na kama taratibu zote za zabuni zilifuatwa na pale ambapo
hazikufuatwa ni hatua gani PPRA wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya
manunuzi na kuleta hasara ya mabilioni ya fedha kwa Serikali.
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha
Dar es Salaam. Novemba 25, 2012
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.