Polisi mkoani Mwanza, imewakamata watu wawili akiwamo afisa wa wanyama pori, Allchraus Jacob (31),na Kasika John (44) ambaye ni mkuluma wa wilayani Bunda, wakijaribu kuuza pembe za kifaru maarufu kwa jina la George (12) akifahamika kama faru wa Rais Jakaya Kikwete, aliyeuawa na majangili, Desemba mwaka jana.#####WAKATI HUO HUO jeshi la polisi mkoani mwanza lanawashikilia watu wanne, wawili kati yao wakiwa na bunduki aina ya SMG na risasi 64 ambazo zilikuwa zimefichwa ndani ya begi la nguo zikisafirishwa kwenda wilayani Geita..
Ndani ya begi hilo kulikuwa na viatu vya kike, panga moja na shoka ambavyo vilikuwa vimefungwa katika mfuko wa sandarusi pamoja na vikaratasi vidogovidogo vilivyokuwa vimefungwa dawa mbalimbali za mitishamba ambavyo walidai kuwa ni hirizi za dawa za kusaidia wakati wa matukio ya ujambazi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment