Mkurugenzi wa Taasisi ya TAASISI ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akiendesha pikipiki inayotumia umeme
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akiendesha bajaji inayotumia umeme
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akizungumzia maendeleo ya mradi huo
Ruta Venance- ambaye ni mhitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Usagara ambayo ni mmoja wa wanufaika na mafunzo hayo akizungumza namna yalivyomsaidia
Na Oscar Assenga, TANGA
TAASISI ya Tanzania Open Innovation Organization ( (TOIO)imesema kwamba itaanza mchakato wa kutengeneza mifumo mbalimbali ya vyombo vya moto mkoani Tanga ambavyo zitasaidia kurahisisha suala la usafirishaji
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Shaukatali Hussein wakati akizungumza na waandishi wa habari katika shule ya Sekondari ya Tanga Ufundi ambalo kunaendelea na mafunzo kwa vijana kuhusu namna ya ubadilishaji wa pikipiki,baiskeli kwenda kwenye mfumo wa kutumia umeme.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi hiyo na Robotech Labs chini ya ufadhili wa Shirika la Botnar Foundation ambao wamedhamiria kutoa ujuzi kwa vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi.
“Kwa kweli tunawashukuru Jiji la Tanga na wafadhili wetu Botnar Foundation sasa tumeweza kuwapa ujuzi vijana kuhusu namna ya kuzibadilisha pikipiki,baiskeli kutoka kwenye mfumo wa awali na kuziingiza kwenye ule wa kutumia umeme hii ni hatua kubwa Alisema
Mkurugenzi huyo aliwataka vijana kuchangamkia fursa ya kupata mafunzo hayo ambayo yatawawezesha baadae kuweza kujiajiri na hatimaye kuweza kuinua uchumi wao na jamii kwa ujumla kwani mpaka sasa ni vijana 30 katika Jiji la Tanga ndio wamenufika na mafunzo hayo na tumetembelea kata mbalimbali mwako ulikuwa ni mkubwa lakini kufika kwenye eneo hilo ni changamoto.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba hivyo wanaiomba jamii na Serikali kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa hiyo muhimu. Lengo likiwa ni kuwapatia vijana hao fursa za kuweza kunufaika na mradi wa kutengeneza pikipiki,baiskeli za umeme ambazo zinatumia betri na mota ya kawaida.
Akielezea kuhusu umuhimu wa vyombo hivyo ambavyo vinatumia umeme alisema ukipa hesabu lita moja ya mafuta ni 2700 unapata kilomita 30 mpaka 40 lakini ukichajisha kwa kutumia umeme ni unit mbili hata 1500 haifiki na unatembea kilomita 90 hivyo inapunguza gharama kwa madereva na inawapatia mtaji mkubwa.
Hata hivyo alisema pamoja na hayo hivi sasa wanaendelea na matengenezo ya Bajaji za umeme walianzia na baiskeli na wakaishia kwenye baiskeli za walemavu na mwakani wataelekea kwenye magari na center ndogo za kutumia umeme.
Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo ni Ruta Venance- ambaye ni mhitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Usagara alisema anashukuru kwamba amenufaika na mradi huo na ujuzi wakutosha alioupata anaweza kutengeneza mwenyewe.
Alisema alimua kutumia muda ambao alikuwa akisuburi kuingia kidato cha tano na sita amejua mfumo mzima wa kutengeneza pikipiki na wanawashauri vijana waliopo mtaani waende kupata mafunzo hayo ni mazuri
Naye kwa upande wake Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya Sekondari Tanga Ufundi Saidi Kasim a,lisema kwamba mradi huo wa utengenezaji wa pikipiki za umeme yatamsaidia yeye na wenzake kuweza kupata ujuzi mbalimbali.
Aidha alishauri kwamba mafunzo hayo yawe endelevu ili waweze kupata ujuzi zaidi huku akiiomba serikali waweze kufadhili mafunzo hayo maana wakifanya hivyo watasaidia kupunguza vitu vingi vinavyoingia nchini kutokana na uwepo wa wataalamu ambao watakuwa na uwezo kuvitengeneza hapa nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.