Na ALBERT G. SENGO
Mwanza.
MKUU wa mkoa wa
Mwanza Eng. Evarist Ndikilo ametoa agizo la siku mbili kwa uongozi wa shule ya
msingi Nyanza kushughurikia suala la vyoo shuleni hapo kwani mazingira hayo sio
rafiki kwa watoto.
Agizo hilo amelitoa leo wakati akizindua mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele katika shule ya msingi Nyanza jijini Mwanza.
Ndikilo amesema kuwa
mazingira ya huduma ya vyoo kwa watoto wa shule hiyo hayaridhishi na ni
hatarishi kwa afya za wanafunzi wa shule hiyo kwani yanaweza kusababisha mlipuko
wa magonjwa ya kuambukiza yanayoambatana na uchafu hivyo amewapa siku mbili wakuu wa shule hiyo
kulitatua suala hilo.
“Kabla sijafika hapa
niliwatuma vijana wangu kuja kuangalia kwanza hali ya mazingira ya shule ikoje
ambayo imepewa kipaumbele cha uzinduzi kwa niaba ya shule zote Mkoani hapa na
ndipo wakanileteta jibu kuwa shule ile ina tatizo la choo kwa wavulana hivyo
naawagiza ndani ya siku mbili watoto wapate pakujisaidia.”alisema Ndikilo.
Aidha kwa mujibu wa
Takwimu zilizotolewa na
Mkurugenzi wa mpango wa taifa wa utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) Dr.Mwela
Malecela zinaonyesha kuwa wakazi wa mkoa wa mwanza wameathirika na ugonjwa wa
kichocho na minyoo ya tumbo kwa 80% huku taifa ikiwa ni 12.7%.
Amesema kuwa ni bora
magonjwa hayo kutibiwa ili
kuhakikisha watoto wanakuwa na Afya njema ili wawe na uwezo wa kuelewa na kuleta maendeleo ya kimapinduzi
katika Elimu.
Mratibu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira akitoa taarifa fupi ya shughuli hiyo ya kitaifa. |
Magonjwa ya Matende na Ngirimaji, minyoo ya tumbo, Kichocho, Trakoma na Usubi ni miongoni mwa magonjwa yanayoathiri jamii na kudhoofisha.
Inakadiriwa kuwa watu bilioni moja duniani kote tayari wameathirika. Zaidi ya watu bilioni mbili wako hatarini kupata maambukizi ya Magonjwa hayo.
Nchini Tanzania tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa maambulkizi ya magonjwa haya hupatikana karibu maeneo mengi.
Kabla ya ugawaji dawa za Minyoo na Kichocho kwa watoto wa shule ya msingi Nyanza, wanafunzi hao walipewa chakula. |
Wanafunzi wa Shule ya msingi Nyanza wakigawiwa chakula. |
Chakula Time. |
Chakula kwanza. |
Safu ya waandishi wa Habari kutoka kushoto ni Mashaka Bartazar wa gazeti la Majira na Jambo Leo, Albert G. Sengo wa Clouds Fm, Hanry Kavirondo wa Channel Ten na kulia ni Mwandishi wa Sahara Media |
Kila mwanafunzi aliagizwa kuja na sahani toka nyumbani hivyo mara baada ya matumizi waliziosha kupitia bomba la shule. |
Pipa la taka katika shule ya msingi Nyanza kwa hisani ya Wizara ya Afya. |
Unyweshaji dawa unaenda sambamba na kujua uzito na kimo cha mtoto. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiendelea kusimamia zoezi la ugawaji dawa. |
Kuna mada imewagusa wanafunzi hawa.... |
Njia ya kujikinga na Magonjwa ya Kichocho, Minyoo ya tumbo, Trakoma, na mengineyo yasiyopewa kipaumbele ni:-
-Kutumia dawa za kutibu na kudhibiti magonjwa ambazo hutolewa kila mwaka kwa jamii iliyoathirika.
-Kuzingatia usafi wa uso na mwili kwa ujumla.
-Kuzingatia usafi wa mazingira kwa ujumla
-Kutokuoga/Kutokuogelea/Kutokutembea kwenye maji yasiyo safi na yaliyotuama kama vile mabwawa na mifereji.
-Kujikinga na kuumwa na inzi, mbung'o, mbu na wadudu wengine wasambazao maambukizi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.