Usiku wa jana umeshuhudia matokeo tofauti katika michezo ya Ulaya, huku Chelsea ikipoteza ugenini, Liverpool ikiwahi dakika za mwisho, na Barcelona ikitoa burudani ya kupindua meza.
Atalanta 2-1 Chelsea
Chelsea imekubali kipigo cha 2-1 dhidi ya Atalanta kwenye mchezo uliochezwa ugenini.
Matokeo:
55’ Gianluca Scamacca (Atalanta)
83’ Charles De Ketelaere (Atalanta)
26’ Pedro (Chelsea)
The Blues walitangulia kupata bao mapema kupitia Pedro, lakini Atalanta walionyesha uimara kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha kisha kuongeza bao la ushindi dakika za lala salama.
Inter Milan
0-1
Liverpool
Liverpool imeondoka San Siro na ushindi mwembamba wa 1-0, bao pekee likifungwa dakika ya 88 na Dominik Szoboszlai.
88’ Szoboszlai
The Reds walionyesha uthabiti mkubwa na subira iliyowalipa mwishoni mwa mchezo.
Barcelona
2-1
Eintracht Frankfurt
Barcelona imepindua matokeo kutoka 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt.
50’ Kounde
53’ Kounde
21’ Knauff (Frankfurt)
Bao mbili mfululizo za Jules Kounde ndani ya dakika tatu ziliipa Barca ushindi muhimu baada ya hiviwana kuanza nyuma.
Tupe maoni yako



0 comments:
Post a Comment