ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, June 22, 2025

TWIGA STARS WATAWAZWA KUWA MABINGWA KOMBE LA CECAFA WANAWAKE

 TANZANIA imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Women’s Challenge Cup baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya Jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Bao pekee la Twiga Stars lililoizamisha Harambee Starlets limefungwa na kiungo mshambuliaji wa Al-Nassr ya Saudi Arabia, Clara Cleitus Luvanga dakika ya 49.
Mchezo mwingine uliotangulia jioni ya leo Sudan Kusini iliichapa Burundi mabao 3-1 hapo hapo Azam Complex.

Kwa matokeo hayo, wenyeji Tanzania wanamaliza na pointi 12 baada ya kushinda mechi zao zote nne, hivyo kutawazwa kuwa malkia wapya wa kandanda ukanda wa CECAFA.

Harambee Starlets inamaliza na pointi tisa katika nafasi ya pili baada ya kupoteza mchezo huo wa kwanza  kufuatia kushinda mechi tatu za awali, ikifuatiwa na Uganda, Burundi na Sudan Kusini ambazo kila moja imemaliza na pointi tatu.

Mshambuliaji Opa Clement Tukumbuke wa Tanzania anayechezea klabu ya wa Juárez ya Mexico ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mabao yake matano akifuatiwa na Martha Emedot wa Kenya aliyemaliza na mabao manne.


Naye kiungo Diana Lucas Msewa wa Trabzonspor ya Uturuki, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa michuano hiyo huku Naijat Idirssa wa JKT Queens akichaguliwa Kipa wa CECAFA Women’s 2025.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment