ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 7, 2016

MTOTO ALIYETENGENEZA JEZI YA MESSI KWA KUTUMIA MAKARATASI AULA.

Murtaza Ahmadi, kijana mwenye umri wa miaka mi 5 shabiki mkubwa wa Lionel Messi picha ya kwanza ikimuonyesha akiwa nyumbani kijijini akicheza soka na kulia ni picha ikimuonyesha akiwa katika moja ya viwanja vya soka mjini Kabul vinavyo milikiwa na Shirikisho la soka nchini humo.
MCHEZAJI BORA DUNIANI ambae huchezea Klabu ya Spain Barcelona, Lionel Messi, anatarajiwa kukutana na Mtoto wa Afghanistan ambae alipata umaarufu Duniani baada ya kupigwa Picha akivaa Jezi iliyotengenezwa kienyeji kwa Mfuko wa Plastiki wa Rangi za Argentina na Jina la Messi huku pia ikiwa na Namba 10.
 
Mtoto huyo mwenye Miaka Mitano aitwae Murtaza Ahmadi anampenda mno Messi lakini Familia yake ya Kimaskini inayoishi Jimbo la Ghazni Jirani na Mji Mkuu wa Afghanistan, Kabul, Nchi ambayo ina misukosuko ya vita, haina uwezo wa kununua Jezi Orijino ya Staa huyo wa Argentina.

Kaka wa Murtaza, Homayoun, mwenye Miaka 15, aliamua kumtengenezea Mdogo wake Jezi ya Argentina kutoka Mfuko wa Plastiki na kuiandika Jina la Messi na Namba 10 kwa Peni na kisha kuiposti Picha yake kwenye Mtandao wa Facebook Mwezi uliopita. Picha hiyo ilizagaa mno Dunia nzima na kuwa maarufu kupindukia. Sasa, Jorge Messi, Baba Mzazi wa Lionel Messi, amesema Lionel Messi anajua kuhusu Picha hizo na anataka kufanya kitu kwa ajili ya Shabiki wake huyo Mtoto wa Afghanistan ikiwa pamoja na kukutana nae.
Ubalozi wa Hispania nchini humo umesema uko tayari kushughulikia tena bure, taratibu zote za visa kwa baba wa mtoto huyo pamoja na mwanae. Alisema Keramuddin Karim, Rais wa Shirikisho  "We are trying to make contact directly with Barcelona to arrange the meeting, where, when and which date."

Murtaza Ahmadi, katika picha ya pamoja na moja ya wachezaji wanaocheza ligi ya Afghanistan.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.