Mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa na hofu kubwa imetanda eneo la tukio kuhofia usalama wa hali za abiria waliomo ndani ya basi husika kwani basi limepinduka tairi zikielekea juu, limetumbukia kwenye majaruba ya mpunga, limepondeka vibaya upande mmoja, na tayari katika muda huu napita eneo la tukio miili ya watu wawili imeonekana ikizagaa nje ya basi kandokando ya barabara na mvua kubwa inaendelea kunyesha.
Hali ya uokoaji imeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili ni wachache tu abiria wameweza kupewa miamvuli na watu walio kwenye magari yanayopita eneo hili ili wapate kujisitiri. |
Chanzo cha ajali kinatajwa kuwa ni mwendo kasi wa busi hilo. |
Watoto wakiwa na mama zao wanalia tu wakihitaji msaada, mvua ikiwanyeshea wakihofia usalama wao na mali zao. |
Baadhi ya nyumba zilizo karibu na eneo la ajali nazo zimeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili wilayani Magu. |
Hali ya baadhi ya barabara za ndani zinazounganisha vijiji wilayani Magu zimefunikwa na maji. |
Barabara hali ya hewa na mazingira. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.