ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, November 14, 2010

SHINYANGA YANG'ARA KTK VODACOM MWANZA CYCLE CHALENGE.

MBIO ZA TANO ZA BAISKELI ZINAZODHAMINIWA NA KAMPUNI YA MAWASILIANO YA SIMU ZA MKONONI VODACOM TZ ZIMEMALIZIKA JANA JIJINI MWANZA.
HAPA NI MSUGUANO MKALI KATI YA WASHIRIKI NAFASI ZA JUU WANAWAKE (YA 1,2,3) PICHANI NI KATIKA ENEO LA IGOMA MZ, AMBAPO WANAWAKE WALISHIRIKI MBIO ZA KILIMETA 80.

LAITI KAMA MSHIRIKI HUYU TOKA SHINYANGA AITWAYE NDYESHIMBI KURYA, ANGEKUWA NA BAISKELI YA KISASA KAMA WENZAKE NA AKAJIFUNZA JINSI YA KUITUMIA, NAAMINI KUWA NDIYE ANGETAWAZWA MSHINDI, KWANI NI KATIKA KILIMA CHA BUGANDO KWENDA KUIMALIZA UNGWE NDIPO ALIPO PITWA NA WENZAKE (MSHINDI WA 1 NA WA 2), NA KUWA MSHINDI WA TATU.

KUTOKA KUSHOTO MSHINDI WA KWANZA SOPHIA EDSON (ARUSHA)ALIYEJINYAKULIA TSH MILIONI 1.1, MSHINDI WA PILI MATHA ANTHONY (MWANZA) ALIYEJINYAKULIA TSH 800,000 NA WA TATU NDYESHIMBI KURYA (SHINYANGA) ALIYEJINYAKULIA TSH 600,000.

MSHIRIKI HUYU TOKA SHINYANGA ALIPATA AJALI KWA BAISKELI YAKE KUCHOMOKA TAIRI LA MELE AKIWA KATIKA MWENDO KASI LAKINI MUNGU SI ATHUMANI HAKUUMIA SANA ZAIDI YA MAJERAHA MADOGO MADOGO.

WASHIRIKI WAKITOKA KWENYE MBIO SUALA LA KUTEMBEA INAKUWA INSHU PLOBLEM.

AKITUMIA BAISKELI YA KAWAIDA MSHINDI WA KWANZA HAMISI CLEMENT KUTOKA SHINYANGA AKIMALIZIA UNGWE KILOMETA 196 WANAUME.

HAMISI CLEMENT MSHINDI WA KWANZA ALIYEJINYAKULIA ZAWADI YA TSH. MILIONI 1.5 TOKA VODACOM.

MSHINDI WA PILI RICHARD LONING'O LAIZER (ARUSHA) ALIYEJINYAKULIA TSH. MILIONI MOJA.

MSHINDI WA TATU SENI KONDA (SHINYANGA) ALIYEJINYAKULIA TSH. 700,000. HUKU MSHINDI WA 4 HADI WA 10 TSH. 500,000 KILA MMOJA, WASHIRIKI WA 11 HADI 20 WALIPATA TSH. 250,000 KILA MMOJA NA WA 21 HADI 30 WAKIJINYAKULIA TSH. 90,000 KILA MMOJA.

NAE MKIMBIAJI WA ZAMANI MBIO HIZO ZA BAISKELI ISAC TAYLOR, AMESEMA KUWA ILIKUNYANYUA MCHEZO HUO NA KULILETEA TAIFA HESHIMA, ANA MPANGO WA KUCHUKUWA VIPAJI ALIVYOVIONA KATIKA MICHUANO HIYO (MWANZA NA SHINYANGA) NA KUVIPATIA MAFUNZO, MBINU NA VIFAA VYA KISASA KAMA BAISKELI, NGUO ZA MASHINDANO NA KADHALIKA AKIAMINI KUWA NI VIPAJI VINAVYOWEZA KUSHINDA HATA MICHUANO YA KIMATAIFA ULIMWENGUNI.

AWALI KABLA ZILIFANYIKA MBIO ZA KILOMETA 10, KWA WALEMAVU AMBAPO WASHINDI WAWILI WA KWANZA WALIPATA ZAWADI YA SHILINGI 400,000 KILAMMOJA NA WENGINE WAWILI WALIOSHIKA NAFASI YA PILI WALIKAMATA SHILINGI 250,000, NAFASI YA TATU WALIKABIDHIWA SHILINGI 150,000 KILA MMOJA NA WANNE HADI 10 WAKIONDOKA NA SHILINGI 70,000 KILA MMOJA. KWA CHATI NYUMA MENEJA WA UDHAMINI MATUKIO YA VODACOM BI. RUKIA MTINGWA (ALIYESHIKA KICHWA) "WAANDISHI WA HABARI MMENIANGUSHA! NEXT TIME NATOA SEMINA KABLA YA MASHINDANO" AKILALAMIKA MARA BAADA YA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI KUONEKANA WAKIWA WAMESIMAMA ENEO LA MSTARI WA KUMALIZIA MBIO, HIVYO KUWAPA WAKATI MGUMU WASHIRIKI KTK UMALIZIAJI.

MAKAMPUNI MENGINE YALIYOJITOKEZA KUDHAMINI NI Alphatel, Knight Support na SBC.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.