LEO ni siku ya Uhuru wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika. Watanzania wote wanaadhimisha uhuru wa Tanganyika kutimiza miaka 49 tangu wakoloni wa Uingereza walipokabidhi hatamu za uongozi wa taifa hilo, ambalo sasa linajulikana kama Tanzania Bara, kwa wananchi wenyewe, Desemba 9, 1961. Maadhimisho ya siku hiyo yanawapa nafasi na changamoto kubwa Watanzania za kutafakari walikotoka, walipo na wanakokwenda li kuona wapi walikosea, kuteleza au kufanya vizuri, na kupanga mikakati ya kuondoa kasoro na kuweka mipango madhubuti zaidi ya kuendelea kulijenga taifa lao.
TATIZO LA MAJI SAFI NA SALAMA.
Yapo maendeleo makubwa yaliyopatikana kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali na wananchi tangu uhuru. Lakini pamoja na maendeleo hayo, zipo changamoto kubwa zilizokwaza harakati hizo za maendeleo, ambazo wakati wa kusherehekea miaka 49 ya uhuru, tunapaswa kuzitafakari na kuzipatia ufumbuzi utakaolipeleka mbele zaidi taifa letu.
MIAKA 49 YA UHURU WA TZ OYEEE..
NINA AMINI KUWA TUTAFIKA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.