ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 10, 2012

THIERRY HENRY AIPAISHA ARSENAL FA

Goli pekee lililofungwa na mkongwe aliyerejea Arsenal, Thierry Henry limeipatia timu hiyo ushindi na tiketi ya kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la FA katika mchezo uliopigwa jana dhidi ya Leeds United.

Henry, 34, alifunga goli lake la 227 kwa Arsenal baada ya kurejea kuichezea klabu hiyo kwa mkopo wa miezi miwili.

Arsenal sasa itakutana na Aston Villa katika raundi ya nne ya kombe la FA katika mchezo utakaochezwa Januari 28.


Boss wa The Gunners Wenger anaronga kuwa: "Ndoto imekuwa kweli, ni hadithi ambayo mara zote nimekuwa nikiwaambia vijana kuhusu mchezo wa soka. "Tayari tulikwisha mtawaza kama Legend wa hapa lakini usiku wa leo kaongeza kitu zaidi katika historia yake yote."

"It didn't surprise me that he scored tonight but when he was through on goal I thought his angle was a bit too close. "But he didn't force his shot and still made it look easy. That was the special finishing of Thierry Henry that we all know."

Arsenal wamesonga mbele baada ya kupata ushindi wa bao 1-0.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.