Katika kilele cha Siku ya wanawake duniani Machi 8 mwaka 2020, kilichofanyika Viwanja vya Shule ya Sekondari Sanjo, Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza, Wanawake nchini wametakiwa kuonyesha kivitendo uwezo na usawa kijinsia kwa kugombea udiwani na ubunge badala ya kubanana kwenye nafasi za viti maalum huku wanawake wengine wakitakiwa kuwaamini na kuwapigia kura wanawake wenzao ili kuleta mapinduzi makubwa.
Mmoja wa waanzilishi wa Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la jijini Mwanza KIVULINI Yusta Ntibashima akizungumza na kusanyiko lililojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani wilayani Misungwi. |
Huenda umeshuhudia siku ya Wanawake Duniani ikitajwa kwenye Vyombo vya Habari au kusikia kwa marafiki .
Lakini kwa nini? Lini? Je ni sherehe au maandamano? na Je kuna siku kama hiyo ya kimataifa kwa Wanaume?
Kwa zaidi ya karne sasa, watu duniani wamekuwa wakisherehekea siku hii.
1. Ilianzaje?
Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura.Kilikuwa chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadae.
Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina Clara Zetkin.+1+0
Alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.
Kwa mara ya kwanza ilisheherekewa mwaka 1911, Austria, Denmark,Ujerumani na Switzerland.
Sherehe ya 100 ilifanyika mwaka 2011, hivyo mwaka huu ni sherehe ya 107 ya wanawake duniani.
2.Ilikuwalini?
Tarehe 8 mwezi Machi. Wazo la Clara Zetkin la Siku ya kimataifa ya wanawake duniani halikuwa na tarehe maalum na haikuwa rasmi mpaka kipindi cha vita ya mwaka 1917 wakati wanawake wa kirusi walipodai Amani na kufanyia kazi tatizo la upungufu wa chakula (Waliimba Amani na Mkate).
Siku nne za mgomo, zilifanya watawala wa Urusi kuwapa wanawake haki ya kupiga kura.Tarehe ambayo mgomo ulianza ulikuwa kwenye kalenda ya Julian, ambayo ilikuwa ikitumika Urusi wakati huo, ilikuwa siku ya Jumapili tarehe 23 Mwezi Februari.
Siku hii katika kalenda ya Gregoria ilikuwa tarehe 8 mwezi Machi.
3.Je kuna siku ya wanaume?
Ndio ipo, tarehe 19 Novemba. Lakini iliadhimishwa tangu miaka ya 90 na haitambuliwi na Umoja wa Mataifa.Watu huiadhimisha katika nchi zaidi ya 60. Lengo la siku hii ni kutazama afya za wanaume na wavulana, kuimarisha mahusiano ya jinsia,usawa wa jinsia na kutathimini jinsia ya kiume kama watu wa mfano wa kuigwa.Kauli mbiu ya mwaka 2017 ilikuwa 'kuwaadhimisha wanaume na wavulana'
OCD wa Misungwi Shabu B. Shabu akitoa darasa. |
Kauli mbiu inayoendesha kampeini ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani mwaka huu ni usawa kwa sawa #EachForEqual, ambayo inaangazia usawa wa papoja.
"Sote ni sehemu ya dunia moja," kampeini hiyo inasema. "Mchango wetu wa kibinafsi, mtazamo, tabia na fikira zetu zinaweza kubadili jamii kwa ujumla.
"Kwa pomoja, tunaweza kuleta mabadiliko. Kwa pamoja, kila mmoja wetu anaweza kuchangia upatikanaji wa usawa wa kijinsia duniani."
Meneja CRDB Misungwi Deogratius Kessy amefunguka kuhusu unyanyasaji wa kiuchumi kwa ufasaha haswaa.. |
Katika miaka miaka michache iliyopita wanaharakati wa kutetea haki za wanawake walipiga hatua kubwa. Mwezi Oktoba 2017, mamilioni ya wanawake walianza kapeini ya #MeToo katika mitandao ya kijamii ili kupinga unyanyasaji na dhulma za kingono.
Mwaka In 2018, kampeini ya #MeToo ilipata umaarufu duniani, huku mataifa kama vile India, Ufaransa, China, na Korea Kusini yakijiunga na kampeini hiyo kushinikiza mabadiliko.
Nchini Marekani, wanawake walivunja rekodi katika uchafuzi wa katikati ya mhula.
Mwaka jana utoaji mimba ulihalalisha Ireland Kaskazini huku sheria inayodhibiti mavazi ya wanawake nchini Sudan ikifanyiwa mabadiliko.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.