Mtaalamu wa Saikolojia, Dr. Chris Mauki, amewahi kuandika kuhusu dhana ya hofu au mashaka. Akitoa ufafanuzi alisema na kusisistiza kuwa, “hofu au woga, ndio adui namba moja anayedhoofisha nishati ya mwili wa mwanadamu kwa haraka pengine kuliko kitu kingine; na kwamba wengi wameshindwa kufikia malengo na ndoto zao katika maisha kwa sababu ya hofu, mashaka na woga.”
Hata hivyo, wapo watu wengine ambao wameelemewa na tabia ya hofu kwa kiwango cha juu sana, kitu ambacho kinawaathiri, na kuwafanya washindwe kufuatilia hata mambo muhimu ya maisha yao.Hofu ni hulka ambayo humpata kila binaadamu, ingawaje kwa viwango vinavyotofautiana.
Kwa mujibu wa historia, hata makamanda wa vita, walioogopwa sana, walikabiliwa na hofu! Waliogopa kushindwa vita, kuchukuliwa mateka au hata kuuawa. Lakini, tofauti ya hawa na wengine, ni ujasiri na hamasa ya kushinda waliyoijenga ndani yao kila siku.
Tunaambiwa na wataalamu kuwa, kama ulivyo wasiwasi na woga, hofu ni athari ya kisaikolojia ambayo hutokana na hisia au mawazo hasi.
Ndio maana Mwandishi John F. Paul anatuhimiza tusitawaliwe na mawazo hasi. Anasema: “Akili zetu hazikuumbwa ili kukaa na hasi, kwani unapokuwa mtu wa kuwaza au kusema hasi, kumbukumbu hizo zinasafirishwa na kuhifadhiwa katika akili (ubongo) ya ndani, na baadaye kudhihirika au kutokea kiuhalisia.”
Kinachowakabili watu wengi, wakashindwa kuanza kufanya biashara ki-vitendo, ni hofu au woga wa kufeli, lakini vilevile wapo wanaoogopa vitu visivyojulikana.
Watu hawa badala ya kufikiria ni kwa namna gani watakabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza, wao wanajenga hofu ya kushindwa na wanaanza kuwaza madhara yatakayowapata watakaposhindwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.