Hayo yamesemwa leo na Naibu wa Katiba na Sheria Ummy mwalimu wakati akizindua mkakati wa usajili wa Vizazi kwa watoto wa chiniya umri wa miaka mitano (U5BRI) mkoani Mwanza.
Mpango huo umelenga kumsajili na kumpatia cheti kila mtoto katika eneo la karibu na mahali tukio lilipotokea kwemye jamii kwa wakati muafaka kadiri inavyowezekana ukiratibiwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini nchini (RITA) ikiwa ni utekelezaji wa haki ya msingi ya mtoto kutambuliwa. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA NAIBU WAZIRI.
Katika mfumo wa kawaida wa maisha, gharama za huduma mbalimbali huongezeka kilasiku, lakini katika mkakati huu Serikali imeamua kuondoa ada ya Cheti kwa watoto hivyo basi haitakuwa na sababu ya watoto kutokuwa na nyaraka hii muhimu kwa maisha yao.
Kwa mujibu wa takwimu za usajili wa watoto nchini, ni asilimia 16 tu ya watoto chini ya umri wa miaka mitano wamesajiliwa na katika hao ni asilimia 7.7 tu wamepatiwa vyeti vya kuzaliwa na kuifanya kuwa nchi iliyo na asilimia ndogo ya wananchi waliosajiliwa kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki. Ambapo Kenya na Burundi usajili upo zaidi ya asilimia 60, Rwanda usajili upo zaidi ya asilimia 80 na Uganda usajili upo zaidi ya ailimia 20.
Usajili wa Mkoa wa Mwanza upo asilimia 13 yaani chini ya wastani wa Kitaifa.
Wakati huo huo Serikali imesema kuwa itatoa Tuzo kwa Waganga wakuu wa Wilaya watakao hamasisha na hatimaye kufanikisha zoezi la kusajili watoto wengi wa chini ya umri wa miaka mitano toka kwenye wilaya zao.
Mwanza ni mkoa wa pili kuhusishwa na mpango huo wa Serikali ulioboreshwa zaidi ukisaidiwa na mfumo wa kujaza takwimu kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi wa Tigo.
Lengo la Serikali ni kuwa ifikapo mwezi Disemba 2015 zaidi ya watoto 400,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wawe wameasajiliwa.
SEHEMU YA HOTUBA YAKE:-
Ndugu Wageni waalikwa,
Sote tunavyofahamu kuwa maisha ya mwanadamu yeyote yanaanzia pale anapozaliwa. Tukio la uzazi, maana yake ni ongezeko la idadi ya watu katika jamii na katika taifa.
Kwa upande wa Serikali tukio hilo maana yake ni kuongezeka wajibu wa kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wake. Ni kwa sababu hiyo, upatikanaji na utunzaji wa kumbukumbu sahihi za kila tukio jipya la uzazi linapotokea ni jambo la msingi sana. Umuhimu wa taarifa hizo ndio umepelekea kuanzishwa kwa Wakala wa Serikali wenye jukumu mahususi la kusajili vizazi na vifo nchini.
Takwimu za Vizazi ni kichocheo cha maendeleo nchini kwani Serikali huhitaji takwimu hizi kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo ya muda mfupi na muda mrefu. Bila takwimu hizi ni vigumu kwa Serikali kuweza kujua kwa usahihi mahitaji ya kupeleka huduma muhimu kwenye jamii. Kwa mfano ni muhimu kujua katika miaka mitano ijayo kutakuwa na wanafunzi wangapi wanaohitaji kuanza elimu ya msingi. Hii itasaidia kujua kama shule katika eneo husika zinatosheleza au la, vituo vya afya vingapi vinahitajika katika eneo husika, nk.
Mkakati wa Usajili wa Vizazi kwa Watoto walio na umri wa chini ya Miaka Mitano tunaouzindua leo hapa Mkoani Mwanza ni utekelezaji wa haki ya msingi ya mtoto kutambuliwa. Nasema hivyo kwa sababu, unalenga kumsajili na kumpatia cheti kila mtoto katika eneo la karibu na mahali tukio lilipotokea kwenye jamii kwa wakati muafaka kadiri inavyowezekana.
Nafahamu kwamba sambamba na Mkakati huu wa Usajili wa Vizazi kwa Watoto Chini ya Miaka Mitano, RITA imeanza mchakato wa kuboresha Mfumo mzima wa usajili na utunzaji wa kumbukumbu za Matukio yote mahimu ya mwanadamu (Civil Registration and Vital Statistics – CRVS) ambayo ni Vizazi, vifo, ndoa na talaka. Vilevile nafahamu pia upo Mkakati wa Usajili wa Watoto Mashuleni ambao umeanza kutekelezwa katika Jiji la Dar es Salaam. Natoa rai kwa RITA na wadau wengine wa Usajili kuangalia uwezekano wa kuziwezesha program hizi zote kufanya kazi kwa pamoja kwani zote zinalenga kuwasaidia wananchi.
Nachukua fursa hii kuwashukuru wadau wote wa maendeleo wanaochangia utekelezaji wa Mkakati huu. UNICEF, DFATD, VSO na Tigo. Serikali inathamini sana michango yenu na tunawaomba muendelee kuisaidia Serikali mara mnapohitajika na mnapokuwa katika nafasi ya kufanya hivyo. Nasema Ahsanteni sana.
Paul Edwin Naibu mwakilishi UNISEF |
Ally Maswanya Meneja wa Mawasiliano Tigo Kanda ya Ziwa. |
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Emmy Harison akitoa maelezo kwenye kusanyiko hilo. |
Katika
utekelezaji wa Mkakati huu katika sehemu zilizotangulia kulikuwa na changamoto
mbalimbali ambazo tumezifanyia kazi na kuzipatia ufumbuzi ili zisiweze kujirudia
Mkoani Mwanza hivyo ni Imani yetu kwamba hapa tutapata matokeo bora zaidi na
kwa wakati.
Katika
utekelezaji Mkoani Mbeya tumeweza kubaini kwamba zipo program mbalimbali katika
sekta ya Afya pamoja na Serikali za mitaa zilizoweza kutekelezwa kwa mafanikio
makubwa hivyo basi Kwa Mwanza na mikoa inayofaya tutaweka msisitizo katika
kufungamanisha usajili wa vizazi na program hizo.
Baada ya
kampeni kukamilika, itafuata awamu ya pili ya kampeni ya kuendelea na zoezi la
usajili na kutoa vyeti katika Vituo vya Tiba vinavyotoa huduma ya afya ya Mama
na Mtoto ili kuwawezesha watoto ambao hawakuweza kusajiliwa katika kampeni na
wale wanaozaliwa kuweza kupata huduma hiyo.
RITA na
wadau inaoshirikiana nao imejipanga kutoa mafunzo ya kina kwa watendaji
watakaohusika katika usajili ambao watajulikana kama Wasajili Wasaidizi. Pia
tutaimarisha Utendaji katika Ofisi za Makatibu Tawala wa Wilaya kwa kuweka
Komyuta na vitendea kazi vingine vitakavyotumika kurahisisha kazi za usajili.
Mkakati huu utatumia teknolojia ya simu na kompyuta katika kutuma na kutunza kumbukumbu hivyo kuendana na kasi ya mabadiliko duniani. Hivyo naweza kusema ni mkakati unaoenda na wakati.
Katika mfumo wa kawaida wa maisha, gharama za huduma mbalimbali huongezeka kila siku, lakini katika Mkakati huu Serikali imeamua kuondoa ada ya Cheti kwa watoto hivyo basi hakutakuwa na sababu ya watoto kutokuwa na nyaraka hii muhimu kwa maisha yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.