ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, August 11, 2019

WAKAZI WA MKOLANI WABAINI FAIDA ZA UNYONYESHAJI WATOTO MAZIWA YA MAMA


WAKAZI wa Mkolani wilayani Nyamagana mkoani Mwanza mwishini mwa wiki wameshiriki darasa la wazi lililofanyika mbele ya eneo la wazi la ofisi ya mtendaji sokoni katani mwao.

UNYONYESHAJI MAZIWA YA MAMA NI FAIDA
Maziwa ya mama husifika kwa  virutubisho vya hali ya juu na vyenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya mtoto mchanga. Baadhi ya virutubisho hivyo ni pamoja na protini, wanga, mafuta na madini ambayo ni muhimu katika ukuwaji wa mtoto mchanga na uimarishaji wa mfumo wa ufahamu.

Vile vile, maziwa ya mama humpatia mototo kinga asilia yenye kumwezesha kupambana na baadhi ya magojwa na maambukizi yakiwemo;

Maambukizi ya sikio na mafua ya mara kwa mara
Magojwa ya mfumo wa chakula yanayopelekea kuharisha, pamoja na magojwa sugu kama crohn’s, celiac na necrotizing  enterocolitis.
Magojwa ya atopic kama eczema na asthma ambayo asilimia kubwa husababishwa na matatizo ya mzio (allergies)

Hupunguza hatari za unene wa utotoni
Hupunguza hatari za kifo cha ghafla kwa watoto wachanga SIDS (Sudden Infant Death Syndrome)

Baadhi ya faida kwa mama anayenyonyesha ni pamoja na kujenga mahusiano ya karibu ya awali kati ya mama na mtoto.   Mama anayenyoshesha husemakana kupunguza hatari za magojwa ya saratani ya matiti na saratani ya ovari. 

Vile vile, tendo la kunyonyesha hupelekea  mwamko wa ongezeko la uzalishaji wa  homini ya oxytocini mwilini. Oxytoxini ni homoni inayohusika na kupelekea mwamko wa uchungu wa uzazi na uandaaji wa mazingira ya kukabiliana na zoezi la uzazi. Pale zoezi hilo linapokamilika  oxytoxini husaidia kufinya au kubana misuli ya tumbo la uzazi na hivyo kupunguza hatari za mama kupoteza damu nyingi na kurudisha tumbo la uzazi katika hali yake ya  awali. (Lawrence,..2005)Shirika linalojihusisha na malezi bora kwa watoto wachanga "American Academy of Pediatrics" (AAP)  lasisitiza  unyonyeshaji wa watoto wachanga  kwa kipindi kisichopungua miezi sita. Mtoto akishatimia umri wa miezi sita, AAP yashauri mtoto kupatiwa vyakula vigumu pamoja na maziwa ya mama ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya mwili. Mtoto anayeachishwa ziwa la mama chini ya umri wa miezi 12 hushauriwa kutumia fomula zilizo na virutubisho vya madini ya chuma na sio maziwa ya ng'ombe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.