Shughuli ya kuwapongeza ilifanyika jana usiku katika moja ya kumbi nzuri za Lakairo Hotel ambapo waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali walipata fursa ya kujumuika ktk hili.
“Nawashukuru sana kwa kuwa mmeisaidia Halmashauri ya jiji la Mwanza kupata heshima katika utumishi sekta mbalimbali na pia kuchangia kuleta amani katika jiji la Mwanza kwa kuwasaidia watendaji wa serikali ngazi zote kufikisha ujumbe wa kile kilichonuwiwa kwa wananchi.” Kauli ya mgeni rasmi.
“Rais hivi majuzi kasema viongozi wa serikali watoe ushirikiano kwa waandishi wa habari ili kusaidia watanzania kujua mafanikio, matatizo yao na mapungufu nao wapate kushiriki au kuchangia katika harakati za utatuzi, Wito kwa mkurugenzi wa jiji la Mwanza aondoe urasimu uliopo wa kutoa habari kwa kutenga siku maalum kwa waandishi kupata habari ili jamii itambue nini kinafanywa na Halmashiauri zake”


Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.