ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 29, 2015

BAADA YA CCM KUPULIZA KIPENGA WATANGAZA NIA YA URAIS WACHUANA.

NA PETER FABIAN, MWANZA.

BAADA YA CCM KUPULIZA KIPENGA WATANGAZA NIA YA URAIS WACHUANA.

*KANDA YA ZIWA YAONGOZA KWA MAKADA WA CCM KUTANGAZA NIA YA URAIS.

*WAZIRI Dkt. MAGUFURI AFUNGUA UTEPE MJINI DODOMA.

*WAZIRI MKUU ALIYEJIHUDHULU EDWARD LOWASSA KUUNGURUMA LEO ARUSHA.

*WAZIRI WASSIRA KESHO KWENYE UKUMBI WA CHUO CHA BENKI KUU (BOT) TAWI LA MWANZA.

MAKADA wa Chama cha Mapinduzi  wanaojitokeza kuwania Urais kupitia Chama hicho wameanza kuchuana kutangaza baada ya vikao vya Kamati Kuu Taifa (CC) na Halmashauri Kuu Taifa (NEC) kumalizika hivi karibuni Mjini dodoma na kutoa baraka zote kuanza rasmi kwa mchakato huo.

Orodha ndefu ya Makada hao hadi sasa walioonyesha nia ya kutangaza kuwania ni ndani ya Chama hicho ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuri (Mbunge wa Chato), Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Masatu Wassira (Mbunge wa Bunda), Profesa Sospiter Muhongo aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini aliyejiudhuru kwa Sakata la Escrow (Mbunge wa Kuteuliwa).

Wengine ni Waziri Mkuu aliyejihudhuru, Edward Lowassa (Mbunge wa Monduli), Waziri Mkuu Mstaafu (1995-2000), Frederick Sumaye, Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mbunge wa Katavi), Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (Mbunge wa Singida Magharibi), Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Taitus Kamani (Mbunge Busega) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benarld Membe (Mbunge wa Mtama).

Wapo Pia Waziri wa Asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya (Mbunge wa Rungwe Mashariki), Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (Mbunge wa Bumbuli), Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Lameck Mchemba (Mbunge wa Ilamba) ambaye hivi karibuni alitangaza kujihudhuru nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa ambaye hivi karibuni , Mbunge wa Jimbo la Sengerema, William Ngeleja, Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dr. Khamis Kigwangalla.

Makada wengine ni pamoja na Spika Msataafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sitta (Mbunge wa Ulambo), Mbunge wa Muleba, Profesa Anna Tibaijuka, Balozi Bi Amina Salum Ali (Zanzibar), Mbunge wa Songea Mjini, Emmanuel Nchimbi na Mtoto wa Baba wa Taifa Makongoro Nyerere (sasa ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki) lakini hodhora hii inaweza kuendelea kuwa ndefu hadi mwisho wa muda uliowekwa.  
         
Pazia la Makada hao limefunguliwa rasmi Mei 28 Mjini Dodoma na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuri mara baada ya kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara yake, alipotangaza kwa waandishi wa habari waliotaka kujua kama atawania nafasi hiyo ya kuliongoza taifa kupitia mchakato na utaratibu wa Chama hicho ambapo utafanyika mchujo kabla ya wagombea watano kupigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Agosti mwaka huu.

Waziri Magufuri ambaye ni mzaliwa wa Wilaya ya Chato mkoani Geita ameeleza kuwa atagombea Urais kutokana na kuamini kuwa anao uwezo, sifa za kuchaguliwa na kuchagua kwa mujibu wa Katiba ya Chama chake na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa Raia wa Tanzania mwenye akili timamu kwa kufuata misingi na taratibu za Chama.

WASIFU WAKE.
Dk. John Pombe Joseph Magufuri alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 wilayan Chato mkoani Geita (zamani Mkoa wa Kagera), alisoma shule ya Msingi Chato mwaka 1967-1974 na kuhamia shule ya msingi Katoke wilayani Biharamulo mkoani Kagera, elimu ya sekondari alisomea Kagera na kumalizia Sekondari ya Lake 1977-1978, mwaka 1979-1981 sekondari ya Mkwawa mkoani Iringa na 1981-1982 alisoma Diploma Chuo cha Mkwawa (Iringa).

Dk Magufuli alipata Shahada ya Kwanza ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kati ya mwaka 1985-1988 katika masomo ya  Kemia na Hisabati, alipata Shahada ya Uzamili kwa somo la Kemia katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na badae Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza kati ya mwaka 1991-1994 na Shahada ya Uzamivu ya Kemia alipata katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kati ya mwaka 2006-2009.

Waziri Dk. Magufuri  aliweza kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alihudhuria na kupata mafunzo katika Kambi ya JKT Makuyuni mkoani Arusha kati ya Julai – Desemba 1983 na JKT Makutupora mkoani Dodoma, lakini pia aliendelea kupata mafunzo hayo katika Kamba ya JKT Mpwapwa mkoani Dodoma kuanzia Machi hadi  Juni 1984.

UZOEFU WA KAZI
Dk. Magufuri aliwahi kuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Sengerma mkoani Mwanza akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati ikiwa ni kuanzia mwaka 1982-1983, alijiunga na Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (NCU 1984 Ltd) kama Mkemia Mkuu kuanzia 1985-1995, aligombea Ubunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki mwaka 1995 na kushinda kwenye uchaguzi mkuu.

Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi mwaka 1995-2000 wakati wa Utawala wa Serikali ya Awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Benjamini Mkapa (Mstaafu), aligombea tena Ubunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na kushinda na mwaka 2000-2005 aliteuliwa tena kuwa Waziri wa Ujenzi baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 ambapo aliteuliwa na Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia 2008-2010.

Uchaguzi wa mwaka 2010 aliposhinda tena Jimbo la Chato, aliteuliwa na Rais Dkt. Kikwete kushika Wizara ya Ujenzi hadi 2015 anapo malizia na kutangaza nia ya kugombea Urais katika utumishi wake wa Uwazir aliwahi kuitwa Askari wa Mwamvuli na Rais Mkapa ikiwa ni pamoja na Rais Kikwete na Waziri Mkuu aliyejuhudhuru Edward Lowassa Mbunge wa Jimbo la Monduli mkoani Arusha.

MBUNGE WA JIMBO LA MONDULI- Bw. EDWARD LOWASSA.
Kada mwingine ni Lowassa ambaye hivi karibuni alisema nyumbani kwake Mjini Dodoma mbele ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini kuwa leo atatangaza nia yake kugombea Urais ndani ya Chama hicho leo Mei 30 mwaka huu katika Uwanja wa michezo wa Shekh Abed Karume uliopo Mjini Arusha na kutangaza vipaumbele vyake na sera za mikakati yake endapo atashinda na kuteuliwa kupeperusha Bendera ya CCM kwa mwaka huu.

Tayari maandalizi ya Mkutano wa leo katika Mji wa Kitalii wa Arusha imedaiwa kufulika kwa washabiki wa Lowassa kutoka kila kona ya nchi hii wakiwemo Makada na viongozi na wanachama wa CCM, Viongozi wa Taasisi za Dini, Makundi ya kijamii, wasanii, wafanyabiashara, watalii na wageni kutoka ndani na nje ya nchi na kuufanya Mji wa Arusha kuwa na wageni na kuwa na uhaba wa nyumba za kulala na kulazimika wengine kulala kwenye magari na mahema.

WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA- WASIRA.
Bw. Steven Masatu Wasira, Kada huyu ni Mbunge wa Jimbo la Bunda na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika katika Serikali ya Awamu ya Nne ya kumalizika kwa Utawala wa Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambaye atatangaza nia yake ya kuwania Urais kupitia Chama hicho ambapo tayari ameweka bayana kutangazia rasmi kufanya hivyo katika Ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania uliopo Capil Point jijini Mwanza kesho Mei 31 mwaka huu.

Wasira ni moja ya wanasiasa wakongwe na wenye weredi wa kupambana na siasa hasa za Wapinzani kutokana na kuonja ladha ya Mageuzi mwaka 1995 akiwania Ubunge wa jimbo la Bunda kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi akichuana na Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba ambaye alimshinda na kufikishana Mahakamani kutokana na kuwepo madai tuhuma za rushwa katika uchaguzi wa mwaka huu.

MBUNGE WA JIMBO LA SENGEREMA- NGELEJA.
Kada huyu tayari yupo Jijini Mwanza katika maandalizi ya kutangaza nia kuanzia wakati wowote ambapo kwa mijibu wa taarifa za awali amedhamilia kutangazia jijini Mwanza kisha kwenda Jimboni kwake kwa lengo la kupata baraka za wapiga kura wake na tayari amesema kwamba endapo hatapata fursa ya kuteuliwa na chama chake kuwania Urais atarejea kuwania Ubunge wa Jimbo la Sengerema.

Wanachama wengine watakao tangaza nia hivi karibuni ni pamoja Makongoro Nyerere (Butiama) Juni 1 mwaka huu, Profesa Muhongo (Musoma) Juni 2 mwaka huu, Waziri Mkuu Pinda hivi karibuni Kijijini kwake Mlale Wilayani Katavi wa Maliasili Nyalandu kutangazia Mjini Singida, Mbunge wa Nzega Dr. Kigwangalla (jimboni kwake) Waziri Dk Kamani kutangazia Busega (Simiyu) na wengine pia wakiendelea kufanya maandalizi ya mwisho kutangaza rasmi kuingia ulingoni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.