ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 30, 2013

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA BIMA TANZANIA YATOA MSAADA KWA KITUO CHA NYUMBA YA WATOTO WAB AFRICA MWANZA

Kamishna wa Bima nchini Israel Kamuzora (kushoto) akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vuandarua na mashuka katika kituo cha Kulelea watoto yatima cha Nyumba ya watoto wa Afrika kilichopo eneo la Igoma jijini Mwanza.
Wadau wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA) walitoa vitu vifuatavyo:-
 Sukari kilo 100
Mchele kilo 100
Unga wa Sembe kilo 100
Vyandarua 100
Shuka pea 100 ambapo ni idadi ya shuka 200
Biskuti kwaajili ya chai na viburudisho vya soda
Vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 3.2
Wafanyakazi na viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania wakishusha msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vuandarua na mashuka katika kituo cha Kulelea watoto yatima cha Nyumba ya watoto wa Afrika kilichopo eneo la Igoma jijini Mwanza.

Ni vyakula kwa kituo..

Ni wadau wawakilishi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima kutoka mikoa ya Zanzibar, Arusha, Dar, na Mwanza.

Matandiko kama shuka na neti ni sehemu ya msaada.

Ni Biskuti kama viburudisho kwa watoto.

Sukari kilogram 100 kwaajili ya kituo.

Kamishna wa Bima nchini Israel Kamuzora amesema kuwa dhumuni la ujio wao jijini Mwanza ni kuhamasisha suala la Umuhimu wa Sekta ya Bima ambapo watoto wanapata fursa ya kuishi bila wasiwasi mara baada ya wazazi wao kufariki dunia either kupitia maradhi au harakati mbalimbali za maisha. 
Wafanyakazi na viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania wakigawa vinywaji kwa watoto wa kituo cha cha kulelea watoto yatima cha Nyumba ya watoto wa Afrika kilichopo eneo la Igoma jijini Mwanza.

Wafanyakazi na viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania wakigawa vinywaji na pipi kama viburudisho kwa watoto wa Kituo cha cha kulelea watoto yatima cha Nyumba ya watoto wa Afrika kilichopo eneo la Igoma jijini Mwanza.

Hakika ilikuwa siku yao njema kufurahi pamoja kwa watoto wa kituo hiki kilichoanzishwa zaidi ya miaka 15 iliyopita, ambapo kwa sasa kina watoto 108.

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Tanzania walipata fursa ya kuzungumza ana kwa ana na watoto wa Kituo cha cha kulelea watoto yatima cha Nyumba ya watoto wa Afrika

Kila mmoja na mtoto wake.

Furaha na watoto.

Picha ya Group.

Neno la shukurani kwa mapokezi yaliyoonyeshwa na watoto na uongozi wa kituo kwa wadau wa Usimamizi wa Shughuli za Bima.

Bango la kituo cha nyumba ya Kituo cha kulelea watoto yatima cha Watoto wa Africa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.