Mwanri ametoa agizo hilo jana katika uzinduzi wa msimu mpya wa kilimo cha pamba uliofanyika kitaifa katika Kijijicha Mwamashimba wilayani Igunga Mkoani Tabora na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa zao hilo kutoka mikoa ilimayo zao la pamba hapa nchini .
BOFYA PLAY
Igunga, 20 Novemba, 2017: Msimu mpya 2017/18 wa kilimo cha pamba katika Kanda ya Magharibi inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Tabora, Mara, Kagera, Singida, Kigoma na Katavi, umezinduliwa rasmi jana ambapo upandaji pamba umeanza rasmi na utaendelea hadi mwishoni mwa mwezi Desemba.
Igunga, 20 Novemba, 2017: Msimu mpya 2017/18 wa kilimo cha pamba katika Kanda ya Magharibi inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Tabora, Mara, Kagera, Singida, Kigoma na Katavi, umezinduliwa rasmi jana ambapo upandaji pamba umeanza rasmi na utaendelea hadi mwishoni mwa mwezi Desemba.
Akiongea katika
uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Marco
Mtunga amesema kwamba katika msimu wa kilimo wa 2017/18 jumla ya tani
25,000 za mbegu zimetengwa zikijumuisha tani 11,548 za mbegu mpya ya
UKM08 na tani 13,452 za mbegu ya UK91. Kiasi hiki kinawahakikishia
wakulima uwepo wa mbegu za kutosha kwa maeneo yote yatakayozalisha pamba
msimu wa kilimo.
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Hadi tarehe 12 Novemba 2017, jumla ya tani 11,056 ambayo ni sawa na asilimia 70 ya mbegu zote zimesambazwa katika maeneo mbalimbali kati ya tani 15,694 zilizopangwa kusambazwa katika mgao wa awali. Zoezi la usambazaji wa mbegu lilianza tarehe 15 Septemba 2017 na limepangwa kukamilika tarehe 30 Novemba 2017.
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Hadi tarehe 12 Novemba 2017, jumla ya tani 11,056 ambayo ni sawa na asilimia 70 ya mbegu zote zimesambazwa katika maeneo mbalimbali kati ya tani 15,694 zilizopangwa kusambazwa katika mgao wa awali. Zoezi la usambazaji wa mbegu lilianza tarehe 15 Septemba 2017 na limepangwa kukamilika tarehe 30 Novemba 2017.
Jumla
ya ekari milioni moja na laki tatu zinatarajiwa kupandwa pamba msimu wa
kilimo 2017/18. Serikali kwa kushirikiana na Wadau imefanikiwa kufufua
mfumo wa kuzalisha mbegu bora za kupanda na kwamba azma ya Serikali ya
kuwapatia wakulima mbegu bora mpya ya UKM08 ifikapo mwaka 2018/2019
itatekelezwa kama ilivyopangwa.
Aliongeza kusema kwamba; Mfumo wa
uzalishaji wa mbegu bora za pamba unaanzia Kituo cha Utafiti cha
Ukiriguru ambapo mbegu mama (Breeder Seeds) inazalishwa na baada ya
kupatikana zinapelekwa kupandwa katika shamba la Nkanziga lililopo
Wilayani Misungwi ili kuzalisha mbegu za awali (Pre-Basic Seeds). Baada
ya hapo mbegu zinapelekwa kuzalishwa na wadau wengine (Quton seed Co. na
Gaki ginnery) katika Kata ya Mwabusalu wilayani Meatu ili kupata mbegu
za Msingi (Basic Seeds).Ngazi ya mwisho ya katika mtiririko wa
uzalishaji wa mbegu iliyothibitishwa (certified seeds) zinazalishwa
wilayani Igunga. Katika msimu wa kilimo wa 2017/18, jumla ya tani 11,548
za mbegu mpya ya UKM08 zinasambazwa katika Wilaya 34 kati ya 48
zinazolima pamba nchi nzima.
Kwa
lengo la kuboresha kilimo cha pamba Serikali imejipanga kueneza
matumizi ya mbegu zilizoondolewa nyuzi ili kwenda sambamba na mataifa
mengine yanayolima duniani kwani kilimo cha pamba duniani kinafanyika
kwa kutumia mbegu zilizoondolewa nyuzi. Katika msimu huu wa kilimo wa wa
2017/18, Mikoa ya Tabora na Mara inapanda mbegu zilizoondolewa nyuzi na
kwamba elimu ya matumizi ya mbegu hizi inaendelea kuenezwa katika
maeneo yote. Lengo la Serikali ni kuwapatia wakulima wote mbegu
zilizoondolewa nyuzi ifikapo msimu wa kilimo wa 2018/19. Zifuatazo ni
faida za Mbegu zilizoondolewa nyuzi:-
• Kuua vimelea vya magonjwa na wadudu hivyo kuzuia kuenea kwa magonjwa
• Mbegu zinatumika kidogo.
• Gharama kidogo za usafirishaji, utunzaji.
• Uwezekano wa kutumia mashine katika upandaji.
• Uhakika wa uotaji kwa kuwa mbegu zisizokomaa, zilizoshambuliwa na wadudu zinaondolewa.
• Ni rahisi kuchanganya na kiuatilifu na kusafisha kwa kuwa inanyumbulika.
Tatizo
la pamba Tanzania si bei wala soko bali ni tija ndogo ya kilo 300 kwa
ekari badala ya kilo 1,000 kwa ekari ambazo wakulima bora wa pamba
wanazalisha kwa sasa. Mkulima wa pamba ataweza kuongeza kipato chake
mara mbili au mara tatu akiongeza tija. Ili kubadilisha hali hii, Bodi
ya Pamba na Serikali kwa ujumla inachukua hatua zifuatazo:
(i)
Kueneza kilimo cha mkataba ili wakulima waweze kupata pembejeo za
kutosha kwa mkopo ili asiyekuwa na uwezo wa kujinunulia pembejeo
asikwame kulima pamba;
(ii) Kufufuliwa kwa mfumo wa kuzalisha mbegu kunawezesha wakulima kupanda mbegu bora zilizothibitishwa na hivyo kuongeza tija
(iii)
Mheshimiwa Waziri Mkuu na Waziri wa TAMISEMI wametoa maelekezo mahsusi
kuhusu usimamizi wa shughuli za zao la pamba katika ngazi zote hususani
utoaji wa huduma za ugani.
(iiii) Aidha wakulima wawezeshaji
4,532, wawili kutoka kila kijiji kinacholima pamba wameainishwa na
wanaunganishwa na mtandao wa wagani ili mashamba yao yatumike kama
shamba darasa. Wakulima wawezeshaji (Lead Farmers) wanazalisha kilo kati
ya 800 na 1,200 kwa ekari.
(v) Serikali imenunua na kusambaza
kamba za kupandia katika Wilaya 13 ambazo zimekithiri katika upandaji
wa pamba kwa kusia na mafunzo yanaendelea kutolewa
Kauli mbiu
tasnia ya pamba ni “MKULIMA KUTOKA MAFURUSHI MATATU HADI MAFURUSHI KUMI
KWA EKARI” maana yake kutoka kilo 300 hadi kilo 1,000 kwa ekari.
“Wakati
sasa umefika wa kila mkulima wa pamba nchini kulima kwa tija ili
kuongeza uzalishaji na kujikwamua kutoka kwenye umaskini kwani katika
uzalishaji wa zao la pamba tija inachangiwa na kuzingatia kanuni za
kilimo bora cha pamba na kupanda mbegu bora. Iwapo mkulima atapanda
pamba kwa mistari na kuzingatia nafasi inayopendekezwa na wataalam
ambayo ni sentimita 90 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 40 kutoka
shimo na shimo, mkulima atajihakikishia kuwa na idadi ya miche
isiyopungua 22,222 kwa ekari ambayo itamwezesha kupata si chini ya kilo
1,000 za pamba mbegu.
Kupanda pamba kwa wakati na
kwa nafasi inayopendekezwa ni kigezo kikubwa cha kupata pamba nyingi na
bora, lakini mkulima unatakiwa uzingatie kanuni zingine katika mtiririko
wa kanuni kumi za kilimo bora cha pamba ambazo ni pamoja na kupalilia
pamba mara kwa mara, kupunguza miche iliyozidi kwenye shamba,
kunyunyizia viuadudu kudhibiti visumbufu vya mimea, kuvuna kwa wakati na
kutenga pamba katika madaraja ya A na B na mwisho kung’oa na kuchoma
moto masalia yote ya pamba baada ya kumaliza kuvuna.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.