Timu ya Bunge ikifanya mazoezi yake mapema leo Aprili 25 kuajiandaa na mchezo huo utakaochezwa keshi Jioni uwanja wa Amani. |
Timu ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania Bunge Sports Club inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo mkali na wa aina yake ambao ni wa kwanza na timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mapema leo Aprili 25.2016 timu hiyo ilishuka katika dimba hilo la Amani na kupasha misuli maalum kwa hiyo mchezo huo wa hiyo kesho ambapo kwa mujibu wa viongozi wa timu hiyo ya Bunge wametamba kuibuka na ushindi wa kishindo.
Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto ametamba kwa timu yake kuibuka na ushindi mnono katika mchezo huo kwani wana mazoezi ya kutosha na pia wamejiandaa kuonyesha uwezo.
“Tunawaomba wabunge wote kutuunga mkono katika mchezo huu kwani tmu imejindaa vya kutosha kuhakikisha tunashinda. Mchezo huu ni maalum kwa ajiri ya kuimalisha Muungano wetu tukufu hivyo tutaendelea kuuenzi na kuukumbatia na sote kwa pamoja tuzidishe Amani” alieleza Mh. Mwamotto.
Kwa upande wake Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani 'Maji Marefu' ambaye ni miongoni mwa viongozi wa msafara wa timu hiyo ya Bunge ametamba timu yake kuibuk na ushindi mnono kwani wamejiandaa kisaikolojia na mazoezi ya kimichezo.
Naye Mbunge wa Nzega Vijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla viongozi wa timu hiyo ya Bunge amebainisha kuwa, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya Saa 12 Jioni kesho Aprili 26.2016 katika uwanja huo wa Amani.
“Mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Utachezwa kesho ni siku ya Kuadhimisha Muungano wa Nchi ya Jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Tunawaomba watu kujitokeza kwa wingi kuuona mchezo huu ambao utakuwa wa aina yake kwa timu zote mbili.” Alieleza DK. Kigwangalla.
Timu hiyo ya Bunge yenye wachezaji Zaidi ya 19 imejiandaa vya kutosha katika kuakikisha inapata ushindi mnono na ipo Visiwani hapa kwa maandalizi ya mchezo huo tokea jana na leo imeweza kufanya mazoezi ya awali asubuhi na mengine wakitarajia kufanya hapo jioni.
Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani 'Maji Marefu' akisimamia mazoeszi hayo kwa muda wakati wsa asubuhi ya leo
mazoezi hayo yakiendelea..
Mazoezi yakiendelea
Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto (kati) akitoa maelezo ya mazoezi hayo
Benchi la ufundi likiwa tayari katika mazoezi hayo
Mbunge William Ngeleja akijaribu kutaka kuchukua mpira kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mazoezi moto moto yakiendelea..
Mazoezi makali ya timu ya Wabunge yakiendelea katika uwanja wa Amaan, Unguja leo Aaprili 25.2016. Timu hiyo kesho Aprili 26 inatarajia kucheza mchezo wao dhidi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog, Zanzibar).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.