Odinga ameliambia jarida la Financial Times la Uingereza kuwa,
ana ithibati ya kuonyesha kuwa mfumo wa matokeo wa Tume Huru ya Uchaguzi
na Mipaka IEBC ulidukuliwa na matokeo yakabadilishwa kwa maslahi ya
Rais Uhuru Kenyatta aliyetangazwa mshindi.
Hii ni licha ya maafisa IEBC kukanusha madai hayo, huku timu za waangalizi wa uchaguzi huo ikiwemo Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki na IGAD zikiisisitiza kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru, wa haki na wazi.
Matokeo rasmi ya IEBC yanaonyesha kuwa, Uhuru Kenyatta aliyegombea kwa tiketi ya chama cha Jubilee alipata ushindi baada ya kujizolea kura zaidi ya milioni nane na laki mbili sawa na asilimia 54.27 ya kura zote, huku Odinga aliyegombea kwa tiketi ya ODM akipata kura zaidi ya milioni 6 na laki saba, sawa na asilimia 44.74 ya kura zote.
Odinga (Kushoto) na Rais Kenyatta
Hata hivyo viongozi wa NASA wanadai kuwa, Odinga alipata kura zaidi ya milioni nane huku Rais Kenyatta aliyewania kiti hicho kwa muhula wa pili akipata kura milioni saba na laki saba.

Taharuki imetanda nchini Kenya huku kila mmoja akisubiri kauli ya Odinga, ambaye alisema hatoenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Katika ghasia za baada ya uchaguzi huo uliofanyika Jumanne ya wiki iliyopita, watu 24 wameuawa kwa kufyatuliwa risasi kwa mujibu wa Kamisheni ya Taifa ya Haki za Binadamu, ingawaje wapinzani wanadai kuwa waliouawa ni watu zaidi ya 100.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.