MNAMO TAREHE 23.01.2017 ,MAJIRA YA SAA 6:40HRS ASUBUHI KATIKA OFISI YA TANESCO MKOLANI KATA YA MKOLANI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA ISSAYA WILSONI JEREMIAH MIAKA 30, MLINZI WA KAMPUNI IITWAYO SUPREME SECURITY GUARD NA MKAZI WA BUGARIKA , ALIKUTWA AKIWA AMEFARIKI DUNIA KWA KUNYONGWA SHINGO NA MTU/WATU AMBAO BADO HAWAJAJULIKANA.
WIZI UMEFANYIKA KWA BAADHI VITU AMBAVYO WALIKUWA WAKIVILINDA KATIKA LINDO HILO AMBAVYO NI TELEVISHENI INCHI 32 FLAT SCREENE AINA ZEC, COMPUTER NNE AINA YA DELL, SCANA MOJA AINA YA DELL, NA KING’AMUZI CHA STAR TIMES.A
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIINGIA KAZINI LINDONI MNAMO TAREHE 22.01.2017 MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONI KATIKA OFISI YA TANESCO MKOLANI AKIWA NA SILAHA AINA YA MARK IV AKIWA NA MWANZEKE AITWAYE YOSAM GABRIEL MIAKA 23, AMBAYE ALIKUWA NA KIRUNGU, NDIPO LEO MAJIRA TAJWA HAPO JUU ALIKUTWA AKIWA AMEFARIKI DUNIA HUKU MWENZAKE ALIYEKUWA NAE AKIWA AMETOROKA.
UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO BADO UNAENDELEA PAMOJA NA MSAKO WA KUMSAKA MLINZI AMBAYE AMETOROKA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI WATU WALIOHUSIKA KATIKA MAUAJI HAYO WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.