Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Anthony Tarimo akifungua rasmi mafunzo ya Mfumo wa Kukusanya Maduhuli ya Serikali (GePG).
Baadhi ya washiriki
wa mafunzo ya Mfumo wa Kukusanya Maduhuli ya Serikali (GePG) wakifuatilia
mafunzo.
Baadhi ya washiriki
wa mafunzo ya Mfumo wa Kukusanya Maduhuli ya Serikali (GePG) wakifuatilia
mafunzo.
Wataalam kutoka
Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mafunzo. Kulia ni Afisa TEHAMA, Jane
Kazoba na anayemfuatia ni Afisa TEHAMA Mkuu kutoka Wizara hiyo, Stellah Nguma.
Washiriki wa mafunzo
ya Mfumo wa Kukusanya Maduhuli ya Serikali (GePG) wakifuatilia mafunzo.
Wizara ya Nishati na Madini imetoa
mafunzo ya Mfumo wa pamoja wa Kukusanya Maduhuli ya Serikali (GePG) kwa Maafisa
Madini na Wahasibu wa Wizara hiyo ili kuboresha shughuli za ukusanyaji
maduhuli.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo
hayo, Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Anthony Tarimo alisema kuwa
mafunzo yamelenga kuwawezesha washiriki kuuelewa vyema mfumo huo ili kuwa na
ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali wenye tija.
Alisema Serikali imeamua kuboresha mfumo
wa ukusanyaji wa maduhuli kuwa wa kielektroniki ili kurahisisha ukusanyaji wa
maduhuli na vilevile kuongeza uwazi miongoni mwa Wizara na Taasisi mbalimbali
za Serikali.
“Kupitia mfumo huu, Serikali inao uwezo
wa kujua maduhuli yote yanayoingia kwa wakati mmoja kwa sababu umeunganishwa na
Wizara na Taasisi mbalimbali,” alisema Tarimo.
Alibainisha kuwa Mfumo huo wa GePG
ulianza kutumika rasmi Julai, 2017 na kwamba kwa upande wa Wizara ya Nishati na
Madini mafunzo ya awali yalitolewa kwa watumishi wa Ofisi ya Madini- Kanda ya
Mashariki ambayo inahusisha ofisi za madini za Dar es Salaam, Pwani, Tanga,
Handeni na Morogoro.
Alisema Mfumo huo ni rafiki na kwamba
utaboresha na kurahisisha ukusanyaji wa maduhuli na kwamba mara baada ya
mafunzo, washiriki watakuwa na uwezo wa kuutumia ipasavyo.
Tarimo alisema mafunzo hayo yanawahusu
Wahasibu, Maafisa Leseni pamoja na watumishi wengine ambao kwa njia moja ama
nyingine wanahusika na utoaji wa hati za madai za malipo mbalimbali.
Aliongeza kuwa, mafunzo hayo yanahusisha
uwasilishaji wa mada mbalimbali kutoka kwa wataalam wa TEHAMA wa Wizara ya
Fedha na Mipango na wa Wizara ya Nishati na Madini na pia yatahusisha
majadiliano ili kuboresha utendaji kazi wa watumishi wanaohusika na ukusanyaji
wa maduhuli.
“Wanasheria pia watawasilisha mada ili
kuelewa vyema mabadiliko katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yaliyofanyika
hivi karibuni,” alisema Tarimo.
Mafunzo hayo ya siku nne yanafanyikia
katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (SUA) na yameanza Agosti 28,
2017 kwa kushirikisha zaidi ya washiriki 100.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.