ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 21, 2017

UHABA WA TAARIFA CHANZO CHA JAMII YA WATANZANIA KUKWAMA KIMAENDELEO.


Serikali imewataka maafisa habari wa mikoa na halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji nchini kutoa taarifa kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka za serikali za mitaa kupitia tovuti ili kuimarisha upatikanaji wa habari kwa jamii.

Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa idara ya habari maelezo DK.HASAN ABBAS wakati akizindua tovuti za mikoa mitano ya kanda ya ziwa pamoja na tovuti za halmashauri za wilaya, miji, manispaa na jiji za kanda hiyo. 

DK.ABBAS amesema kuwa matumizi ya tovuti yataiwezesha jamii kuelewa mipango mbalimbali ya serikali na hivyo kuwaondolea wananchi adha ya kufuata baadhi ya huduma katika ofisi za mamlaka za serikali za mitaa.

Kwa upande wao,Baadhi ya maafisa habari wa halmashauri na mikoa ya kanda ya ziwa wameiomba serikali kuwapatia vitendea kazi ili waweze kutimiza wajibu wao wa kuhabarisha umma kupitia tovuti.

Kabla ya kuzinduliwa kwa tovuti hizo,maafisa habari na maafisa Tehama wa mikoa ya mwanza,kagera,mara,simiyu na shinyanga pamoja na wa halmashauri za mikoa hiyo walipatiwa mafunzo ya siku nane ya namna ya kutumia tovuti yaliyotolewa na ofisi ya rais TAMISEMI kwa kushirikiana na mradi wa uimarishaji wa mifumo ya serikali PS3. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.