ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 24, 2017

MAMIA YA MAASKOFU WAJUMUIKA JIJINI MWANZA KUWEKA MIKAKATI YA KUFUFUA UCHUMI AFRIKA MASHARIKI

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonald Masalle, kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, akifungua Kongamano la Maaskofu wa Jumuiya ya Makanisa ya Kiinjilisti Ulimwenguni Agape WUEMA kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, linalofanyika kwa siku mbili (leo na kesho) Jijini Mwanza.
 Askofu Mkuu wa Agape WUEMA barani Afrika, Mande Wilson, akionyesha picha za makanisa mbalimbali ya Kiinjilisti Afrika mashariki kuonesha hali ya uduni iliyopo kwenye maeneo hayo, hali ambayo haiendani na mapinduzi ya teknolojia ya sasa, Wadau wa AGAPE wamenuia kubadilisha mazingira na kuboresha hali za watumishi wa Mungu sanjari na waumini wao.
Kongamano hilo limelenga kujadili na kuazimia mgawanyo wa ujenzi wa miradi ya jumuiya hiyo katika nchi sita za Afrika Mashariki na Kati (Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Kongo) ambayo ni pamoja na Makanisa, Shule na Hospitali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa mataifa husika.
Askofu Mkuu wa Agape WUEMA Tanzania, Martin Gwilla, akizungumza kwenye kongamano hilo.
Askofu Mkuu wa Agape WUEMA Afrika Mashariki Kadoi Frank akizungumza kwenye kongamano hilo.
Askofu Mkuu wa Agape WUEMA Kenya, Kibedi Steven Kibedi, akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi baada ya ufunguzi wa kongamano hilo. Zaidi ya hapo alitoa ufafanuzi kuwa hili ni Kongamano la Maaskofu wa mikoa ya Kanda ya Afrika Mashariki tu  ambapo kwa ujumla madhumuni ya kusanyiko hilo ni kuieneza injili sanjari na kuisaidia jamii ya nchi husika kujenga nyumba za ibada, nyumba za watumishi wa Mungu, kujenga shule na hospitali, nyumba za watoto yatima, wazee wasiojiweza na kadhalika.
Engo nyingine ya viongozi mbalimbali wa jumuiya ya Agape WUEMA
Sehemu ya viongozi mbalimbali wa jumuiya ya Agape WUEMA
Wakifuatilia kwa umakini hii ni sehemu ya Maaskofu mbalimbali wa jumuiya ya Agape WUEMA
Maaskofu mbalimbali wa jumuiya ya Agape WUEMA kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.
Kwaya iliyokuwa ikiamsha kwenye kusanyiko hiyo la Maaskofu mbalimbali wa jumuiya ya Agape WUEMA kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.
Pale neno la \mungu kwa njia ya uimbaji linapo wagusa Maaskofu wa jumuiya ya Agape WUEMA kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kati hakuna wa kuzuia mibaraka ya bwana.
Barikiwa.
Marafiki wakutanapo.
Haya ni mapinduzi katika Taasisi za Kidini nchini ikiwa ni hatua ya kuiga mifano ya mataifa ya nchi zilizoendelea ambapo taasisi zake majukumu yao yamebadilika sasa na kuelekezwa katika kusaidia kwa hali na mali familia zinazoishi mazingira magumu na kuzikwamua kiuchumi kwa kuzijengea uwezo wa kuwa wazalishaji na siyo tegemezi.

Na sasa utamaduni wa mapinduzi hayo unakuja taratibu nchi za  Afrika yakianzia na Jumuiya ya Agape WUEMA kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Kati

Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na taasisi hizo.


Katika risala ya Mkuu wa Mkoa iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonald Masalle kwenye ufunguzi wa kongamano hilo linalofanyika Jijini hapa, amesema serikali inaunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na jumuiya hiyo katika kufanikisha utekelezaji wa miradi yake nchini ikiwemo ujenzi wa makanisa, shule pamoja na hospitali.

"Pamoja na kwamba mnatoka mikoa mbalimbali Serikali inaamini kuwa mtazingatia maadili ya kazi yenu na maandiko matakatifu na sivinginevyo" Kisha akaongeza

"Serikali za nchi zenu ninaamini zimetoa uhuru kuhusu masuala ya dini almuradi uhuru huo hautasababisha kuenenda kinyume na sheria za nchi husika, kama mlivyosema ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu, ni kwamsingi huo viongozi wa taasisi mnazo ziongoza zinathaminiwa sana katika kila nchi kutokana na mchango mkubwa kutoka kwenu kwa masuala ya kiroho na ya kijamii, Haya sasa twende tukazisaidie jamii zetu bega kwa bega na Serikali kwa matendo"


Askofu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Martin Gwila, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake ikiwemo kuruhusu ujenzi wa miradi iliyokusudiwa ambapo ameomba ushirikiano huo kuwa endelevu kwani miradi hiyo itaongeza chachu ya maendeleo katika jamii.

Askofu Mkuu wa Jumuiya ya AGAPE WUEMA barani Afrika, Mande Wilsoni, amebainisha kwamba kongamano hilo lililowakutanisha zaidi ya Maaskofu 170 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati limenga kuhakikisha ugawaji na utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa unaanza mapema mwaka huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.