Na Annastazia Maginga,Mwanza.
KUFUATIA tuhuma za kuwepo kwa dawa ya usingizi ya kuuwa wadudu wa zao la pamba mfuko wa maendeleo wa zao hilo (CDTF) umesema tuhuma hizo sio za kweli badala yake umeongeza uthibiti wa dawa zenye nguvu kwa msimu huu wa pamba.
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella wakati wa ziara yake kwenye kituo cha utafiti wa Kilimo (Ukiriguru)aliuambia mfuko huo kuwa msimu uliopita ulikuwa ukinunua dawa za usingizi na kuwapa wakulima kwa ajili ya kuulia wadudu matokeo yake ilikuwa haifanyi vizuri kutokana na kwamba ilikuwa haiuwi.
Aidha baada ya malalamiko hayo Meneja wa mfuko huo Essau Mwalukasa akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alieleza kuwa tuhuma hizo sio kweli kwani mfuko hununua dawa zilizothibitishwa na taasisi ya utafiti wa viuatilifu (TPRT) ikiwemo kituo cha utafiti wa Kilimo (Ukiriguru) kwenye utathimini ambazo zinakuwa na cheti cha uthibitisho kuwa zinauwa.
Meneja huyo alisema licha ya kuwepo kwa malalamiko hayo mfuko umeanza kuyafanyia kazi ili msimu huu yasitokee na kuwaumiza wakulima na kwamba wameongeza uthibiti wa dawa zenye nguvu ambapo wanatarajia kununua chupa laki tano zitakazogharimu Shilingi billion 2.195 zikiwemo gharama za usafirishaji kwa ajili ya dawa za kuuwa wadudu wa zao la pamba ili kuongeza tija katika mikoa inayolima zao hilo.
“Tuhuma hizi sio za kweli kwa sababu mfuko ni mnunuzi na sijui taarifa hizi zimethibitishwa na nani kwa sisi tunanunua dawa zilizothibitishwa na TPRT zenye cheti maalumu kama hazina cheti kinachothibitisha basi sisi kama mfuko hanunui dawa hizo kama ni kweli hizo dawa ni za usingizi wanaotakiwa watupe taarifa ni wataalumu lakini malalamiko hayo tuliwapatia wakasema watarudisha majibu ndani ya wiki mbili wafanye uchunguzi kwenye maabara zao lakini pia tumeanza kuyafanyia kazi.”alisema Mwalukasa.
Alieleza kuwa dawa inayotupiwa lawama ya usingizi ni ninja ambayo walitumia chupa elfu 88 kati ya laki mbili lakini baada ya kufahamika kuwa haiuwi waliirudisha kwenye kampuni ya muktar iliyokuwa imepewa zabuni ya kununua dawa hizo na kwamba msimu huu kampuni hiyo haijachukuliwa kutokana kutokidhi vigezo.
Aidha alieleza kuwa dawa yenye uthibitisho kwenye msimu huu ni Infectido itakayonunuliwa chupa laki moja badala ya ninja iliyoleta matatizo msimu uliopita itakayogharimu Shiling bilioni moja na zingine zitakazonunuliwa ni Perfecto, Duduba, Ladx, Batherin na Genaral.
“Jumla ya dawa tutakazotumia msimu huu ni chupa laki tano na zina nguvu ya kuuwa wadudu na kampuni tuliyoipa zabuni ni Tata Afirka yenye dawa ya Infectido na perfecto badala ya Muktar ambayo ilikuwa na dawa ya ninja na kampuni zingine ni Entosav pamoja na Bajuta Tanzania Internation”alieleza Mwalukasa.
Alieleza kuwa kwa mwaka jana walipanga kununua chupa laki saba lakini laki mbili mbili zilirudishwa baada ya kuleta matatizo hivyo zikabaki chupa laki tano ikiwemo ninja zilizogharimu Shilingi bilioni 3.5 zikiwemo za usafirishaji kupeleka kwa wakulima.
Hata hivyo aliziomba halmashauri kuchukua jukumu la kutoa mafunzo kwa bwana shamba jinsi ya uchangaji wa dawa ili waweze kuwaelimisha wakulima kwani zikichanganywa vibaya kuna uwezekano wa kutoua wadudu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.