Watoto wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili either na Baba, Mama, Mjomba, Shangazi, Kaka, Dada au mtu yoyote wa karibu ambaye hatarajiwi kufanya vitendo vya ukatili "Kuongea pekee hakutosaidia bali kuchukuwa hatua ndiyo silaha katika vita dhidi ya ukatili..." BOFYA PLAY SIKILIZA ALICHOSEMA
Ni mzazi gani yuko tayari kuona mtoto wake akiadhibiwa na mtu baki? "tutakumbuka fedha tulizo gharamikia kwenye kliniki, tutakumbuka uchungu ulivyokuwa wakati wa kujifungua na kusema huyu ni wakwangu na si wetu...!" BOFYA PLAY KUSIKILIZA
Bi Angelina Benedicto kutoka Shirika la WOTE SAWA akiwasilisha mada inayohusu Utumikishi wa watoto na Upatikanaji wa Elimu Bora. |
HALI HALISI YA SERIKALI ZA MITAA.
Pamoja na akwamba Serikali za Mitaa zinatambulika na Katiba ya Jamhuri ya Muungano kama inavyoeleza muundo na kazi za Serikali hii katika ibara ya 145 na 146 ya katibu ya Jamhuri ya Muungano, bado muundo na utekelezaji wa serikali hii si huru kama zilivyo serikali nyigine hususan Serikali ya Jamhuri ya Muungano na hivyo kupelekea kwa kiwango kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Hii inadhihirishwa na malalamiko ya juu ya viwango vya chini vya huduma za jamii ngazi ya jamii na changamoto za kiutendaji na uongozi zinavyoelezewa na viongozi na watendaji wa Halmashauri mbalimbali hususan utata wa kimiundo, kuingiliwa kimaamuzi, uwalakini kwenye mipango shirikishi na kutokuwa huru kwenye Mapato na Matumizi ya Rasilimali.
Pamoja na changamoto tajwa mara nyingi wengi wa viongozi wa Serikali za mitaa wameshutumiwa kuwa hawawashirikishi wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao kutokana na ukweli kwamba hakuna vifungu vya kikatiba ambavyo vinawabana kufanya hivyo.
Mdahalo wa Wadau wa Elimu katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika wilaya ya Nyamagana uliofanyika katika ukumbi wa JB Belmont Mwanza. |
Afisa wa Eelimishaji toka Shirika la kutetea haki za mama na mtoto (KIVULINI) Bi. Khadija Liganga akiwasilisha mada. |
Afisa wa Eelimishaji toka Shirika la kutetea haki za mama na mtoto (KIVULINI) Bi. Khadija Liganga . |
Ukubwa wa tatizo la ukatili dhidi ya watoto limechangiwa vipi na malezi yetu kwa watoto? Wazazi/walezi wanauelewa gani kuhusu masuala ya mawasiliano na jinsi watoto wao wanavyoyatumia? Watoto wanafahamu mbinu za kujilinda wenyewe dhidi ya ukatili? Wazazi / Walezi wanauelewa kiasi gani kuhusu sheria na haki za mtoto?
Haya ni maswali ambayo familia pamoja na wadau wanapaswa kuyafanyia kazi ili hatimaye kuwa na malezi bora ambayo yataimarisha Taifa letu. Sasa hivi tunashuhudia wimbi kubwa la watoto wa mitaani. Je kama Taifa tumejipangaje kukabiliana nalo? Watoto wa kike wanaozwa na kupata mimba wakiwa na umri mdogo sana na hivyo kukosa haki ya kupata elimu na hivyo ndoto ya kuwa na maisha bora inapotea, nini kifanyike?.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.