WASICHANA 45 walioacha shule na kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali Jijini Mwanza ikiweo kujifungua wakiwa na umri mdogo na kuwa mama wadogo wamewezeshwa vifaa vya ujasiriamali na Kampuni ya Pepsi (SBC) ili kumudu majukumu ya kulea na kujikwamua kiuchumi na familia zao.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa. |
“Nipongeze Shirika lisilo la kiserikali la Education For Better Living (EBLI) nchini chini ya uongozi wa Mkurugenzi wake Benard Makatya kwa uthubutu wa kuanzisha mpango unaolenga kuwajengea uwezo watoto wa kike walioacha shule ili kuwapatia mafunzo mbalimbali yakiwemo ya Kompyuta , Ujasiriamali na Biashara,”alisema.
Shirika hili liko kwa malengo ya kupunguza idadi ya wasichana waaoachishwa shule kutokana na kubebeshwa mimba, kuwawezesha kiuchumi wasichana wadogo na kuwafundisha mbinu za ujasiliamali pamoja na masoko.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo, Meneja wa SBC Mwanza Nicolaus Coetz na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula. |
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akizungumza na umma uliofika kwenye hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi kwa akinamama wajasiliamali jijini Mwanza. |
Meneja wa Kampuni ya SBC Mwanza watengenezaji wa vinywaji jamii ya PEPSI akitoa neno la ufafanuzi kuhusu kampuni yake ilivyojipanga katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii. |
Wakifurahia jambo kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo, Meneja wa SBC Mwanza Nicolaus Coetz na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula. |
Ndikilo alisema mradi huu umeonyesha kufanikiwa na unakuwa chachu ya kuwapatia mabinti nafasi nyingine (Second chance) hasa baada ya kuwa wamepoteza nafasi ya kupata elimu ya kawaida kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni.
Aidha katika kutekeleza mpango wenu wa “Kijana chagua Maisha” unaotekelezwa katika shule 10 za Jiji la Mwanza utasaidia kuwaelimisha vijana wa kike ili waweze kuepukana na mimba za utotoni na kusaidia kuendelea vyema na masomo shuleni.
“Mpango huu niupongeze mnaoufanya kwa ushirikiano baina ya EBLI na Kampuni ya SBC uliolenga kuwawezesha wamama wadogo (Young Mothers) waweze kujitegemea na kufanya biashara ili kupata kipato na kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na utunzaji mazingira ya Jiji letu linaloshikiria rekodi bora ya ushindi wa usafi na mazingira kwa mara ya tisa sasa,”alisema.
Awali Mkurugenzi mwanzilishi wa Shirika la EBLI Mmissional kutoka Maryknoll Lay Marekani, Michael Leen, alisema Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali ya EBLI ilisajiliwa mwaka 2009 nchini na kuweka malengo ya kuisaidia jamii kwa kuanzisha mradi wa kwanza wa biashara ya vikundi unaolenga kuwafundisha au kutoa elimu ya mbinu mbalimbali za biashara na ujasiriamali.
Leen alisema mradi wa pili ni uanzishwaji na uendeshaji wa biashara za vikundi na utekelezaji wake kitumia kwa ambapo utekelezaji wake utashuhudia wanawake 25 wakipatiwa vifaa aina ya Push Carts na wanawake 20 kupatiwa Ice box, meza na viti vyake ili kuboresha biashara na kuongeza tija katika uendeshaji wa shughuli zao.
“Vifaa hivi pia vitawasaidia kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi na vitumike pia katika maeneo yaliyokusudiwa ili visiwe chanzo cha uchafuzi wa mazingira ya Jiji letu hivyo mtatakiwa watunzaji wazuri wa mazingira mkizingatia rai iliyotolewa kwenu na Mkuu wa Mkoa Mhandisi Ndikilo kwenu kabla ya kuwakabidhi vifaa hivi leo,”alisisitiza.Picha ya pamoja baada ya makabidhiano. |
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya SBC, Niclous Coetz, inashirikiana na jamii na kwa kuzingatia hilo imekuwa ikirudisha kwa jamii faida inayopata kupitia bidhaa zake za Pepsi ambapo mbali na kutoa vifaa hivyo itachangia gharama za utoaji elimu na uainishaji wa fursa za biashara na nyanja mbalimbali kwa kushirikiana na EBLI nchini.
Wito wangu kwa wananchi kuendelea kutupatia ushirikiano na kutuunga mkono kwa kununua na kutumia vinywaji vya Pepsi ili Kampuni ya SBC nayo iweze kurejesha faida yake kwa jamii kwa kuchangia miradi na shughuli mbalimbali ya maendeleo na kutoa msaada wa vifaa na kughramia wataalamu wa kutoa elimu ili kuwasaidia wananchi kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.