ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 22, 2013

FAINALI ZA BALIMI NGOMA ASILI ZILIVYONOGA KATIKA PICHA

Kiongozi wa kundi la ngoma la Mwana Lyaku akicheza na nyoka wawili, kundi hili ndilo liliibika washindi wa Balimi Ngoma Festival lililofanyika jana jumapili uwanja wa Polisi Mabatini, na kupeleka shangwe wilayani Magu mkoaniMwanza. 

Kundi la Ngoma la Mwana Lyaku kutoka wilayani Magu ambao ni mabingwa wa Balimi Ngoma Festival 2013 wakisutumuka na minogo ya ngoma yao asili kabila la kisukuma huku mmmoja kati ya vinara wao akicheza na nyoka ambaye mwisho wa siku alimng'ata eneo la karibu na jicho. 

Kuna lugha maalum ya kuwatuliza wakaingia kwenye sanduku lao. Kiongozi wa kundi akiwarudisha bandani na hapa alikuwa tayari kesha ng'atwa. (Ngoja nimsogeze karibu umwone) 

Tizama vizuri jicho la kulia damu zinaonekana na kwamujibu wake kiongozi huyu anasema kuwa anayodawa ya kuondoa sumu fasta....

Kundi linaitwa Mabulo ya Jeshi lilitoa burudani tosha hali iliyoshawishi meza kuukuwatunuku nafasi ya tatu na kunyakua kitita cha shilingi laki 6 fedha taslimu toka kwa wadhamini TBL Balimi Extra Lager.

Kundi la Utandawazi toka wilayani Ukerewe lilinyakuwa nafasi ya pili na kujinyakulia kitita cha shilingi laki 8 na elfu hamsini.

Mwenge sanaa Group walikabiriana na ushindani mkali hatua iliyo wasukuma mpaka nafasi ya nane.

Sapota wa Mwenge sanaa group akiwa angani.

Kundi la ngoma asili la Mwanajilunguja toka mkoani Shinyanga lilitoa burudani tamu sana nakuitwaa nafasi ya saba.

Kundi lililonyakua nafasi ya tano ni Egumba Group aka Gari Kubwa toka mkoani Mara likionesha makali yake uwanjani.

Kama ulikosa tizama waliokuwepo.

Makeke we wacha tu...

Ngoma ya mavuno....

Pepeta...

Kundi la Mwanajilunguja.

Makeke ya Ngoma ya washindi kundi la Mwanalyaku toka Magu Mwanza.

Hapo patamu..

Suala la mavazi na mwonekano wa sare lilizingatiwa na lilikuwa kigezo kimoja wapo kupata ushindi.

Kiasili zaidi...

Vuta subira soon utajionea video ya hawa jamaa waloibuka washindi.
Washindi:-
1. Mwana Lyaku - Magu
2. Utandawazi - Ukerewe
3. Mabulo ya Jeshi - Magu
4. Bujora - Mwanza
5. Egumba group - Mara
6. Magereza - Tabora
7. Mwanajilunguja - Shinyanga
8. Mwenge sanaa Group - Tabora
9. Rugu - Kagera
10. Abagamba Kamo - Kagera

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.