ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 26, 2012

PINDA KUONGOZA MAZISHI YA MWALIMU WA MWALIMU J.K NYERERE

Enzi za uhai wake marehemu Mzee James Irenge ambaye alikuwa mwalimu wa baba wa taifa Julias Kambarage Nyerere katika shule ya Msingi Mwisenge, amefariki akiwa na umri zaidi ya miaka 120 na ameacha watoto 12, wajukuu 30 na vitukuu 15.
Na. Shomari Binda: Musoma

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda amewasili Mjini Musoma mchana huu kwa ajili ya kuongoza viongozi wa Serikali katika kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Mwalimu wa Mwalimu Nyerere mzee James Irenge aliyefariki dunia nyumbani kwake maeneo ya Mwisenge katika Manispaa ya Musoma.

Katika uwanja wa ndege Mjini musoma waziri pinda amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara john Tuppa,waziri wa nchi ofisi ya Rais Stevin wasira,mbuge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Wananchi.

Mzee Irenge, aliyekuwa na umuri wa miaka zaidi ya 120, alimfundisha Mwalimu Nyerere katika Shule ya Mwisenge, kati ya mwaka 1934-1936. Hadi mauti yanamfika,

licha ya umri wake mkubwa, bado alikuwa na uwezo wa kusoma na kuandika mwenyewe bila kutumia miwani wala kusaidiwa.

Wiki kadhaa zilizopita, aliandika barua yake ya mwisho kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akimshuru kwa kumwezesha kumlipia fedha za dawa na chakula mambo yaliyokuwa kilio chake cha siku nyingi.

Mwalimu James Irenge atazikwa katika kijiji cha Busegwe kilichopo katika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara jioni ya leo.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.