ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 3, 2012

BBC YAGONGA MIAKA 80 HEWANI

Shirika la BBC World Service linasherehekea miaka themanini ya matangazo yake ya kimataifa.

Siku ya kwanza ya matangazo ya himaya ya kiingereza BBC ilianza rasmi matangazo yake mwezi Disemba mwaka 1932 kwa redio ya masafa mafupi.

Hotuba ya Mfalme
Siku sita baada ya kufunguliwa rasmi kwa idhaa ya himaya ya kiingereza, ndio ulikuwa mwanzo wa utangazaji, huu ndio ulikuwa ujumbe wa Krismasi wa himaya ya Uingereza. Hotuba ilitolewa na Mfalme George wa tano, moja kwa moja kutoka katika nyumba ya familia ya kifalme ya mapumziko Norfolk mjini Sandringham. Maneno hayo yaliandikwa na mshahiri na mwandishi Rudyard Kipling na hivvi ndivyo hotuba ilivyoanza: " Nazungumza nanyi kutoka nyumbani kwangu maneno haya yakitoka rohoni mwangu." Hivi ndivyo mkurugenzi mkuu wa wa BBC John Reith aliandika katika kitabu chake cha kumbukumbu: " Huu ndio ulikuwa ufanisi mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya BBC. Mfalme alisikika kote duniani.

Vive le Gerale
Serikali ya UIfaransa ilisalimu amri kwa utawala wa Nazi wa Ujerumani mwezi Juni mwaka 1940. Kiongozi wa vuguvugu la 'Free French' Generali Charles De Gaulle, alipeperusha matangazo hadi nchini Ufaransa, kutoka chumba cha matangazo cha B2, katika Broadcasting House. Wafanyakazi waliambiwa kuwa generali ambaye hakutajwa, alikuwa anakuja Broadasting House. Hata hivyo hotuba yake haikurekodiwa na ilibidi kurejelewa, kitu kilichomkera generali huyo. Aliendelea kutangaza kwa dakika tano kila usiku kwa miaka minne. Kulingana na mwandishi mmoja wa idhaa ya kifaransa, hakuwahi kusikia generali huyo akikosea hata kidogo katika matangazo yake. Alikuwa mkarimu na kila baada ya matangazo alimshukuru fundi wa mitambo.

War of words
Ofisi za BBC ziliweza kupatikana Broadcasting House, Oxford Street na katika Senate House. Idhaa mpya ya kimataifa sasa iliweza kupata nguvu baada ya serikali ya Uingereza kugundua umuhimu wa utangazaji. Mwaka 1941, kulikuwa na zaidi ya wafanyakazi 1400. Mwaka huo mbunge wa eneo bunge la Derby, Phillip Noel_Baker, katika mjadala bungeni, alisema "sidhani waziri atatofautiana nami nikisema kuwa katika njia zote alizonazo za kuwafikia watu barani Ulaya, utangazaji ndio njia bora zaidi."


Kuhamia Bush House
Nafasi ya utangazaji kwa idhaa nyingi za BBC, ilikuwa inapungua kule Broadcasting House. Wakati bomu la kutegwa ardhini lililipuka nje ya Broadcasting House mwaka 1940, ilisababisha moto uliodumu saa kadhaa na kusababisha uharibifu mkubwa. Idhaa za Ulaya zikalazimika kuhamia Maida Vale kaskazini magharibi mwa London ambapo walitangazia kutoka kwa chumba kidogo. Mwaka 1941, idhaa hizo zilihamia Bush House, katika barabara ya Fleet Street kitovu cha viwanda vya kuchapishia magazeti wakati huo ikitozwa kodi ya pauni thelathini kila wiki.

Ishara za siri
Wakati wapiganaji waliokuwa wanapinga vikosi vya kigeni barani Uropa, walipojaribu kukabiliana na vikosi hivyo, idhaa hiyo iliwatangazia ujumbe wa siri. Ujumbe huo haukueleweka mfano ''Le lapin a bu un aperif'' ( kwamba sungura alikunywa kinywaji cha aperitif), au '' mademoiselle caresse le nez de son chien'' ( kwamba mademoiselle anapapasa pua la mbwa wake). Huu ujembe ulikuwa unaawambia wapiganaji kuwa ikiwa oparesheni ilikuwa iendelee au ikiwa imesitishwa au ikiwa watu ama stakabadhi zilikuwa zimefika.

Waandishi wa Bush House
Kutoka mwaka 1941 hadi mwaka 1943, George Orwell alifanya kazi kama mtayarishaji wa kipindi katika idhaa ya mashariki. Hakufurahia kazi yake na ilipofika mwaka 1944, aliandika "huenda nikarejelea maisha yangu, na kuweza kuandika kitu muhimu. kwa sasa mimi ni kama chungwa ambalo limekanyagwa na kiatu kichafu sana" Lakini kazi yake katika BBC ilimsaidia kuweza kuandika kitabu chake, mwaka 1984 ambacho inasemekana alitoa mawazo yake mengi kutoka maisha yake BBC.

BBC wakati wa vita baridi
Baada ya vita baridi, uhusiano na utawala wa Strelin ulianza kudorora huku ukuta wa chuma ukiwekwa kati yao. Februari mwaka 1946, wizara ya mambo ya kigeni ya Uingereza, iliitaka BBC kuanzisha idhaa ya kirusi na mwezi mmoja baadaye ikaanza kupeperusha matangazo yake. Mwanzoni wasikilizaji wa Urusi waliweza kusikiliza idhaa hiyo bila wasiwasi lakini punde vita baridi vilipokuwa vinaendelea, serikali ya Urusi ikaanza kudhibiti hali. Matangazo yalianza kuingiliwa, hitilafu za kila mara zikiripotiwa na hivyo BBC ikalazimika kuongeza nguvu za mitambo yake.

Kuhifadhi uwazi.
Wakati wa kutangaza mzozo wa Suez mwaka 1956,waziri mkuu wa Uingereza Anthony Eden, aliamini kuwa idhaa ya kiarabu, inapaswa kutangaza kwa kupendelea majeshi ya Uingereza. Idhaa hiyo nayo iliendelea kutangaza bila mapendeleo kwa usaidizi wa mkurugenzi mkuu Ian Jacob licha ya wizara ya mambo ya kigeni kusema kuwa itapunguza mamilioni ya dola ambazo BBC ilikuwa inapokea kama ufadhili. Katika wiki chache zilizofuata, licha ya vitisho vya waziri na wabunge, BBC ilisisitiza msimamo wake ya kutopendelea upande wowote.

Mageuzi ya Transista
Miaka ya tisini, ilikuwa miaka ya kueneza umiliki wa redio, hasa baada ya kuzinduliwa kwa betri ambazo zingewezesha transista kufanya kazi. Kati ya mwaka 1955 na 1965, umiliki wa redio ulipanda katika nchi za kikomunisti mashariki mwa Ulaya na kuongezeka hata maradufu mashariki ya kati, China , nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na nchini India. Mwezi Mei mwaka 1965, iligeuzwa na kuwa World Service kuweza kuonyesha umaarufu wake wa maswala ya dunia.

Kuhusu vitabu vya kijasusi mwaka 1978, mwandishi katika idhaa ya Bulgeria, Georgi Markov alipokuwa anaelekea kazini Bush House, akiwa katika eneo la Waterloo Bridge. Alihisi uchungu katika paja lake. Alipogeuka alimwona mtu akiokota mwavuli lakini Markov aliendelea na safari yake kwenda Bush House. Baadaye siku hiyo aliugua na kufariki siku tatu baadaye. Uchunguzi uliofanyiwa mwili wake uligundua kidude kidogo katika paja lake. Inaamika kidude hicho kilikuwa na sumu kali. Ilibainika baadaye kuwa polisi wa siri wa Urusi waliunda mwavuli ulioweza kumdunga mwathirika simu hiyo.

Elimumwendo ya Lugha
Katika historia yake, BBC imepeperusha matangazo yake katika lugha 68. Nyingi ya Lugha hizi zimekuwepo na kwenda ikiwemo, Maltese, Gujarati, Kijapani, na Welsh iliyotumika kwa ajili ya idhaa ya Potagonia. Kuanguka kwa ukuta wa Berlin, ilikuwa ishara ya enzi mpya Ulaya Mashariki na BBC ikawa sio muhimu sana kwa watu wa nchi hizo kama ilivyokuwa mwanzoni. Kwa hivyo nyingi ya idhaa za nchi hizo zikafungwa ili kuweza kufadhili vitengo vingine vya BBC ikizingatiwa bajeti yake ambayo ilikuwa inapungua. idhaa hizo zikafikishwa 28 zikipeperusha matangazo yao kupitia mtandao tu.

Habari za uetendeti
Wakati tawala za Kisovieti zillipoporomoka miaka ya tisini, kulikuwa na eneo jipya lililokuwa linatokota katika Ghuba. Tarehe 2 mwezi Agosti, mwaka 1990, majeshi ya dikteta wa Iraq, Sadam Hussein walivamia Kuwait. Wakati uvamizi ulipoanza, mwezi Januari mwaka 1991, World Service, iliondoa mpangilio wa vipindi ili kuweza kupeperusha habari na kuweza kuzungumzia maswala ya dunia kwa mara ya kwanza.

Sifa kutoka kwa Gorbachev
Wakati Mikhail Gorbachev aliposhikwa kwa siku tatu nchini Urusi, Agosti mwaka 1991, mawasiliano yake na dunia ilikuwa tu kupitia idhaa za kimataifa za redio. aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa World Service John Tusa, alikumbuka mkutano wa waandishi wa habari ambapo Gorbachev alisema kuwa BBC ilisikika kwa uzuri na ilishinda redio. zengine. Ina maana kuwa sifa zilitolewa kwa BBC kwa ujumla na kwa idhaa ya kirusi.

Jukumu lisilofaa la Redio
Redio ilikuwa na jukumu kubwa sana katika matukio nchini Rwanda mwaka 1994. Redio Mille Collines, redio ya Rwanda, ilichochea chuki na uhasama kati ya Watutsi na Wahutu. BBC ilisaidia, kutuliza hali kufuatia ombi la mashirika ya misaada. wasimamizi wa vipindi kutoka idhaa za Kifaransa na kiswahili, walisaidiana na shirika la msalaba mwekundu kuwasidia mamilioni ya watu walioachwa bila makao na vile vile kutoa taarifa kuhusu watu waliopotea. Idhaa hiyo baadaye iliweza kupanuliwa na kuwa idhaa ya maziwa makuu.

Hatua za haraka
Tarehe kumi na moja mwaka 2001, wakati mashambulizi yalitekelezwa dhidi ya jumba la World Trade Centre nchini Marekani, waandishi katika Bush House mara moja walipigwa na butwaa hali ikawa ya taharuki. Mhariri msaidizi Rachel Harvey alilazimika kusimama juu ya dawati lake ili kutuliza waandishi na punde kutoa mwelekeo wa namna ya kupeperusha habari hizo kwa siku nzima. 29 Februari, 2012 - Saa 12:28 GMT

Televisheni ya kimataifa
Idhaa ya kiarabu ilianza kupeperusha matangazo yake kupitia televisheni mwezi Machi mwaka 2008, na kufuatiwa na idhaa ya kifarsi mwaka uliofuata. Haikuwa mara ya kwanza World service kutangza kupitia televisheni. Matangazo ya televisheni ya kimataifa ya kiingereza yalianza mwaka 1991kupitia televisheni ambayo baadaye iliitwa World TV mwaka 1996 na kisha sasa inaitwa BBC World News

Utangazaji wa chanzo kwa watu
Wakati wa tetemeko la ardhi nchinin Haiti ishaa ya BBC ya visiwa vya Caribbean, ilitangaza kipindi cha dakika ishirini kila siku kwa lugha ya Haiti, kuweza kutoa taarifa muhimu kuwasaidia watu kuweza kupokea maji na chakula pamoja na dawa baada ya tetemeko hilo lililotokea tarahe kumi na mbili Januari mwaka 2010. Kando na kutoa taarifa za usaidizi kwa waathirika wa tetemeko hilo, kipindi kiliwasaidia watu kuweza kuwasiliana na jamaa zao waliokumbwa na tetemeko hilo. Pia kilitoa fursa kwa wanamuziki wa kigeni kuwafikia waathirika wa tetemeko .

Mtandao wa kijamii.
Wakati wa mapinduzi ya kiraia katika nchi za kiarabu, mwaka 2011, mitandao ya kijamii uligeuka na kuwa chanzo muhimu cha habari kwa waandsihi wa habari katika eneo hilo. Matukio mawili yalionekana kuwa muhimu sana. Mwanzo mitandao hiyo ilibainika kuwa chanzo kikubwa cha habari kwa waandishi wa habari, pili, kupeperusha habari hizo kulifanya wasikilizaji kuwa sehemu ya habari za BBC World Service na namna ambavyo BBC inakusanya na kupeperusha habari zake. 29 Februari, 2012 - Saa 12:28 GMT

A Jolly Good Show
Novemba mwaka 2010, kiongozi anayepigania demokrasia, nchini Syria, ung San Suu Kyi, aliachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani nchini Burma. Katika mahojiano baadaye, alisema kuwa alisikiliza BBC World Service, wakati wa kuzuiliwa kwake na kusema kuwa pamoja na vipindi vingine alipenda kusikiliza kipindi cha ombi la muziki cha A Jolly Good Show ambacho huendeshwa na DJ Dave Lee Travis. Alisema kuwa kusikiliza kwake kwa BBC kulimkamilishaia mtukio duniani.

Nyumba mpya
Mwaka 2012 BBC World Service, inahamia katika jumba la Broadcasting House ila tu wakti huu limefanyiwa ukarabati wa hali ya juu na kuwa jumba la kifahari la matangazo yake baada ya miaka sabini na moja katika Bush House. Waandishi wa habari wotw sasa watakuwa katika jumba moja na wafanyakazi wengine wa BBC mfano waandishi wa mtandao pamoja na wenzao wa Televisheni ili kuweza kuweka habari za kimataifa katika kitovu kimoja.

Habari zote kwa hisani ya bbc swahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.