ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 17, 2013

MWENYEKITI WA ZAMANI WA CCM MKOA WA MWANZA ALIYEUWAWA KUZIKWA SIKU YA ALHAMISI

Marehemu Clement Mabina.
MAZISHI ya aliyekuwa mwenyekiti wa CCM na Diwani wa Kata ya Kisesa wilayani Magu Clement Mabina, aliyeuawa kikatili na kundi la wananchi, yanatarajiwa kufanyika Alhamisi.
 
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia ya marehemu Mabina, Timothy Gregory ambaye ni mdogo wa marehemu, alisema kwamba, mipango ya mazishi imekamilika na zaidi ni pamoja na kusubilia mtoto wa kike wa marehemu aliyoko njiani kutokea nchini Uingereza marehemu waliokuwa nje ya nchi.
 
Gregory alisema, Kijana mdogo wa marehemu (mtoto ) tayari amewasili jana jioni, hivyo mazishi marehemu Mabina yatafanyika kesho kutwa Kisesa wilayani Magu baada ya mtoto wake mkubwa wa kike kuwasili kutoka Uingereza.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi hayo, Henry Matata ambaye ni Meya wa Manispaa ya Ilemela, amesema kuwa, taratibu za maziko ya marehemu Mabina, zinaendelea kufanyika nyumbani kwa marehemu na kupokea wageni mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wanasiasa wa Kada mbalimbali kutoka vyama vya siasa na serikali pamoja na ndugu na rafiki wa karibu na marehemu wa sehemu tofauti nchini kote na nje ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
“Marehemu Mabina atazikwa rasmi Alhamisi saa 7:00 mchana katika shamba lake kulekule Kitongoji cha Kanyama alikouawa. Tayari tumerudisha mabango ya kuzuia watu waliokuwa wakichimba mawe na mchanga kwenye eneo hilo, yaliyoondolewa na kundi la watu waliomshambulia na majirani wamepokea na kudai eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na marehemu kihalali kwani serikali ya kijiji ililikabidhi kwa marehemu kupitia mkutano wa hadhara hali iliyodaiwa kumuua ilikuwa kumuonea na ilitawaliwa na siasa zaidi kuliko uhalisia wa madai ya kundi la watu hao wachache .” alidai Matata.
 
Hadi sasa, mamia ya waombolezaji wakiwemo ndugu, jamaa, wananchi wa Kisesa, wana CCM na viongozi mbalimbali wa Chama na serikali walikuwa wakiendelea kumiminika nyumbani hapo kuomboleza.
 
Nacho Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza, Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo  kimetoa pole kwa wananchi wa Kisesa wakiwemo ndugu na jamaa wa familia za marehemu Mabina na mtoto Temeli Malimi (12) aliyeuawa  kwa kupigwa risasi na marehemu huyo wakati wa purukushani za kujiokoa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Desidery Kiswaga alisema kwamba, marehemu Mabina aliyekuwa Mweneykiti wa zamani wa CCM mkoa wa Mwanza, atazikwa kwa heshima zote stahili.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Sasa kama serikali ya kijiji ilikuwa imeshatoa umiliki na kuitisha mkutano wa hadhara wa wananchi na kutoa kibali,hawa wanaosemekana ni wananchi wa eno hilo la Kanyama walitoa wapi jeuri na maamuzi ya kumvamia na kusababisha yote haya.Kweli sheria ichukue mkondo wake

    ReplyDelete
  2. Jamani hapo katika tukio hili kuna. Utata mkubwa sana,kuna viongozi wa serikali ya kijiji kutoa hati miliki kimya kimya bila kushirikisha wananchi,na kama wananchi wangekuwa wanatambua ivo kusingetokea yote hayo
    Pia kesi ilikuwa bado mahakamani kwa nini marehemu aliamua kwenda kupanda mitia?!
    Kuna mambo mengi ya kujiuliza hapo na kutafakari
    Pia nahakika mauaji yametokea baada ya wananchi kupandwa na hasira marehemu alivyomuua mtoto,kwa nini marehemu atumie risasi kutuliza watu?!kwani ndo kibali cha kumiliki silaha kinasema ivo?!
    Angetumia busara tu,baada ya kuona watu wameleta fujo angeondoka na kwenda kuripoti katika vyombo husika lakini kutokana na ubabe wa viongozi wetu aliamua kutumia silaha ndo chanzo cha yote hayo
    Jamani tujitahidi kutumia busara.katika maamuzi sio tutumie kofia tulizonazo Za uongozi kufanya tutakayo.
    Haya mmewakamata wananchi waliomuua Mabina na yeye kamuua mtoto nani anawajibika?!
    Tusiwe vipofu wa fikira jamani

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.